VALENTINE'S DAY. HISTORIA, MAANA NA ASILI YAKE
Ikiwa zimebaki siku sita kufikia ile sikukuu maarufu ya wapendanao maarufu kama valentine's day. Leo
nimeona niongelee kidogo kuhusiana na hii sikukuu ni vema kila anae adhimisha akaijua siku hii kwa asili yake na akatambua kuwa anapokuwa sehemu
ya Valentine Day anakuwa ana adhimisha nini na kwa sababu gani, wengi
tunasherehekea kama sio kuadhimisha Valentine pasipo kujua asili yake.
Historia ya sikukuu ya Valentine na muanzilishi wake yaani mtakatifu
valentine imejaa utata mwingi.Tunajua kwamba kwa miaka mingi mwezi wa
pili umesherekewa kama mwezi wa mapenzi na hasa siku hii Valentine
sikukuu hii ya valentine tunaweza sema asili yake ni mchanganyiko wa
sikukuu ya kikristo na sikukuu itokanayo na mila za Kirumi (ancient
roman empire) ni vyema tujue mtakatifu valentine ni nani na anahusiana
vipi na mila za kirumi,au laa,basi pande hizi mbili zakutana vipi kuwa
kitu kimoja.
Kanisa la Roman katoliki linawatambua watakatifu watatu walioitwa Valentine au Valentinus, Ambao wate waliteswa na kuuwawa kwa kukataa kuikana imani yao ya kikristo.Inasemekana kwamba Valentine alikua ni padri wa kanisa la Roman enzi zile za mwaka wa tatu za utawala wa kirumi.Wakati ambao mfalume Claudius wa pili aliona kwamba wanaume ambao hawajaowa ni wanajeshi bora kuliko wanaume walio owa ,hivyo alipitisha sheria iliyozuia wanaume kuowa. Lakini Valentine aliona sharia hiyo haikua na haki, akaamua kuvunja sheria ya mfalme na kuendelea kufungisha ndoa za vijana wapendanao kwa siri. Mfalme aliposikia habari zake aliamuru auwawe.
Inasemekana kwamba wakati Valentine amefungwa akisubiri hukumu ya kifo ndipo alipotuma salam zake za kwanza za ‘Valentine’ baada ya kumpenda kimapenzi binti kipofu ambae alikua ni mtoto wa Bwana jela, Binti huyo alimtembelea gerezani mara kwa mara wakati wa kifungo chake. Inasemekana kwamba kabla hajauwawa Valentine alimuandikia binti huyo barua na mwishoni aliandika”Kutoka kwa Valentine wako” kwa lugha ya kigeni “from your Valentine”Msemo ambao hata leo bado unatumika pale mtu anapotuma salam za valentine kwa maandishi. Ingawa bado kuna utata juu ya ukweli kuhusu muanzilishi wa sikukuu ya valentine, kila hadithi utakayo sikia juu yake inaonyesha alikua mtu mwenye Huruma,shujaa,na zaidi ya yote ni mtu aliependa kuonyesha mapenzi.Kutokana na sifa zake,kati ya karne ya tano na ya kumi na tano Valentine alikua moja kati wa watakatifu wenye jina kubwa sana nchini Uingereza na Ufaransa.
Asili ya siku ya Valentine:
Wakati kuna watu wanaamini kua sikukuuya valentine inasherekewa katikati ya mwezi wa pili kama kumbukumbu ya kifo cha mtakatifu Valentino kilichotokea kwenye miaka ya AD 270-Wengine wanadai kwamba kanisa la kikristo liliweka sikukuu hiyo katikati ya mwezi wa pili katika juhudi zao za kuibadili sikukuu ya Lupercalia kua sikukuu ya kikristo. Lupercalia ilikua ni sikukuu ya wapagani iliyosherekewa na wafugaji kati ya tarehe 13 na 15 ya mwezi wa pili, ni matambiko yaliofanyika ili kuondoa roho wachafu katika mji na kukaribisha afya njema na uwezo mzuri wa kurutubisha,sherehe hizi ziliku rasmi kwa ajili ya mungu wa kilimo wa kirumi aliyeitwa Faunus.
Katika sikukuu hii,walichinja Mbuzi na Mbwa kama kafara,na damu ya mbuzi ilipakwa kila mtaa, ngozi ilichovywa katika damu kisha kila mwanamke na shamba lilipigwa kibao na ngozi hiyo yenye damu,wakiamini kua kufanya hivyo kutafanya mwanamke awe na uzazi mzuri na mashamba pia yatatoa mazao mazuri mwaka utakaofuatia.Na jioni baada ya matambiko hayo mabinti ambao hawajaolewa waliweka majina yao ndani ya kibuyu katikati ya mji na baadae kila kijana ambao hajaowa alichagua jina moja kutoka kwenye kibuyu ,jina ambalo alipata ndio mwanamke ambae alitakiwa kumuowa mwaka uliofuatia.Hapa ndipo dhana ya rangi nyekundu wakati wa sikukuu ya valentine ilipotokea
Sikukuu ya Valentine’s: Siku ya wapenzi
Mwishoni mwa karne ya tano,Sikukuu ya Lupercalia ilifutwa ki sharia kwani ilikua na maadili yasio ya kikristo.Papa Gelasius aliitangaza rasmi tarehe 14 ya mwezi wa pili kama sikukuu ya mtakatifu Valentine,yaani Valentines day.Miaka michache baadae sikukuu hiyo ilibeba maudhuhi au uzito wa mapenzi zaidi.Kati ya karne ya tano na karne ya kumi na tano,nchini Uingereza na Ufaransa, iliaminika kwamba tarehe 14 ya mwezi wa pili ilikua ndio mwanzo wa kipindi cha ndege kutaga mayai na hatimaye watoto wa ndege kuanguliwa, hii ilijenga dhana kwamba siku ya sikukuu ya valentine lazima iwe siku ya kuonyesha mapenzi (romance).Ndio maana ndege hutumika kama alama ya Valentine.

No comments:
Post a Comment