BUNGE LA KATIBA, LISSU ASEMA:"MAKABRASHA ALIYOPEWA HAYANA NYARAKA
Mh Tundu Lissu
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu, amesema makabrasha waliyopewa hayana baadhi ya nyaraka, ambazo wajumbe wa Bunge hilo walipaswa kupewa kwa mujibu wa sheria.
Miongoni mwa nyaraka, ambazo wajumbe hawajapewa ni pamoja na zile zinazohusu watu walioajiriwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Lissu alisema hayo baada ya Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Thomas Kashililah, kwa kushirikiana na maofisa waandamizi wa Bunge, kuwapa wajumbe maelekezo ya awali juu ya mazingira ya ukumbi na huduma zinazopatikana katika maeneo ya Bunge.
Alisema nyaraka pekee walizopewa ni katiba mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, rasimu ya katiba mpya pamoja na taarifa ya takwimu.
Lissu alisema nyaraka, ambazo hawajapewa zimeelezewa kwenye kifungu cha 19 (1) (a), (b) na (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2013.
Kifungu hicho kinasema: “Kwa msingi wa mahojiano na uchambuzi uliofanywa kwa kuzingatia vifungu vya 17 na 18, Tume itatayarisha ripoti itakayokuwa na: muhtasari wa maoni ya wananchi kwa kila hadidu ya rejea; mapendekezo ya Tume kwa kila hadidu ya rejea; ripoti za wataalamu waelekezi ambao Tume iliwatumia.”
Dk. Kashililah alisema nyaraka, ambazo wajumbe wanapaswa kupewa ni nyingi na kwamba, zote zinachapishwa, zikikamilika wajumbe watapewa.
Rimmmmmaaaaaa
ReplyDeleteMamaaaa naona umekuja kivingine, e bwanaaa ,
i wish to be one of the contributors of this blog @Rimma, Grant me access pliz
ReplyDelete