BINADAMU JITAMBUE:
Makala maalum kuhusu maisha
Kutambua ndani yako hakuhitaji uende
shule na kusoma sana,na hakutokani na maamuzi ya mtu mwingine bali ni maamuzi yatokayo
ndani mwako
Ni
mguso unaotaka ndani mwako, ufahamu unaokua toka ndani mwako. Ni
uchimbuzi wa chemchem zitokazo ndani mwako, Ni kumtambua Mungu kupitia
mguso ndani ya moyo wako, kisha kuanza kutumia kipawa ulichonacho kwa
ajili ya utukufu wa Mungu . Ni hisia za ndani zitakazofanya umfahamu
Mungu na si kufikiria
tu.Upya ndani ya binadamu hutokea wakati wote
kwa kuunganisha moyo wako na ulimwengu wa hisia na kuendelea kujifunza
kila wakati na kukuza nafasi ya moyo wako kuwa mpya.
na
Je ni kwa namna gani unamtambua binadamu anayejitambua?
Mtu anayejitambua hubadili mtazamo
wake kutoka kwenye mtazamo wa jamii unaofuata mila na desturi/kawaida kuelekea kwenye fikra za
kuijenga dunia mpya na yenye fursa mpya.Hujenga dunia ambayo wanaomzunguka ni
wanadamu wanaotambua utu na nafasi ya kila nafsi.Akiwa na misingi ya ujamaa na
usawa, hufanya majukumu yake kutoka kujitazama yeye binafsi na kuanza
kuwatazama wengine.Uchaguzi wake na matendo yake husukumwa na maono na mtazamo wa mbali kwa ajili ya
binadamu wote na viumbe vyote.Hutazama sio kila kiumbe kwa ajili yake,bali kila
kiumbe kwa ajili ya wote.
Anayejitambua habagui jinsia bali
hutambua jinsia kuwa ni matokeo ya fikra za Mungu yaliyokusuduia kutoa
fursa.Huheshimu, hutambua wengine na kuthamini nafsi zao na uchaguzi
wao.Hutengeneza dunia dunia ambayo jinsia zote huwa na uhuru wa kutumia vipawa vyao, kutambua sauti zo,nuru
ndani mwao na kutumia kwa ajili ya viumbe wote.
Mtu anayejitambua hasukumwi kutenda
na maamuzi ama fikra za wengine. Anatazama ndani yake.Hajifananishi na nafsi
zingine na hivyo hatumii nafasi yeyote kuwakandamiza wengine.Husimama kwa miguu
yake mwenyewe. Anawasikiliza wengine isipokuwa hatoi nafasi kwa wengine
kumuamulia maisha atakayoishi. Anayaona mambo yajayo na hivyo huanza kuijenga
kesho yake katika wakati tunaouita sasa. Ni alama ya uwezo wa Mungu uliopo
ndani ya binadamu. Na alama ya maisha yake huishi enzi na enzi.
Mtu anayejitambua huchukua hatua juu
ya hisia zitokazo ndani mwake na hivyo kutambua matokeo ya matendo
yake.Hutenda kwa msukumo wa moyo. Hutambua mambo ambayo hayamletei faida na
kutoyafanya na pia hutambua yale yanayomletea faida ..akitambua kuwa
anapotenda kwa wengine anajitendea mwenyewe. Husikiliza hisia za ndani mwake na
kujifunza lugha ya moyo wake.
Huishi maisha yenye sababu. Husikia
muito alioitiwa na kuuuishi. Haridhishwi tu na maisha ya tokanayo na matukio
kama kuamka,kutembea,kulala,kula bali hutambua kuwa yupo hapa duniani kwa
sababu maalum,hivyo huchimba ndani mwake kuijua sababu na kuiiishi. Kila wakati
anasukumwa na sababu hiyo ya yeye kuishi ,kuendelea kuishi kwa dhati akitengeneza na kuifuata njia
inayomfikisha huko.
Hakimbii majukumu yake . Hajitoi
katika kutafuta suluhu ya changamoto na wala halaumu wengine. Hutambua makosa
yake na kujifunza kupitia hayo. Husanifu maisha yake na kuyafanya mapya kila
wakati.
Hujifunza toka ndani mwake na kutoka
kwa wengine. Hutilia mkazo katika mafanikio ya ukuaji ndani mwake kuliko
mafanikio ya nje., hutengeneza ndani mwake. Hutafiti na kuvumbua chemchem
zinazojenga na kubomoa nafsi na kutumia chemchem hiyo kuifanya dunia kuwa
sehemu bora ya kuishi.Hivyo aliyejitambua ni picha tosha ya uwezo na uwepo wa Mungu ndani ya binadamu.
Hutengeneza msawazo kati ya chemchem ndani mwake na matokeo yaonekanayo
halisia.;
- See more at: http://pongujoseph.blogspot.com/2013/09/sifa-za-binadamu-anayejitambua.html#sthash.2otJTs9x.dpufLeo katika makala ya elimu na maisha tunajifunza juu ya binadamu anayejitambua.Makala hii inaweza kukukumbusha mambo mengi kwa kifupi na hivyo kukufanya uchunguze juu ya maisha yako na kuyatumia vyema kwa wakati huu ulipo hapa duniani.
Kutambua ndani yako hakuhitaji uende shule na kusoma sana,na hakutokani na maamuzi ya mtu mwingine bali ni maamuzi yatokayo ndani mwako
Ni mguso unaotaka ndani mwako, ufahamu unaokua toka ndani mwako. Ni uchimbuzi wa chemchem zitokazo ndani mwako, Ni kumtambua Mungu kupitia mguso ndani ya moyo wako, kisha kuanza kutumia kipawa ulichonacho kwa ajili ya utukufu wa Mungu .
Ni hisia za ndani zitakazofanya umfahamu Mungu na si kufikiria tu.Upya ndani ya binadamu hutokea wakati wote kwa kuunganisha moyo wako na ulimwengu wa hisia na kuendelea kujifunza kila wakati na kukuza nafasi ya moyo wako kuwa mpya.
na
Je ni kwa namna gani unamtambua binadamu anayejitambua?
Mtu anayejitambua hubadili mtazamo wake kutoka kwenye mtazamo wa jamii unaofuata mila na desturi kawaida kuelekea kwenye fikra za kuijenga dunia mpya na yenye fursa mpya.Hujenga dunia ambayo wanaomzunguka ni wanadamu wanaotambua utu na nafasi ya kila nafsi.Akiwa na misingi ya ujamaa na usawa, hufanya majukumu yake kutoka kujitazama yeye binafsi na kuanza kuwatazama wengine.Uchaguzi wake na matendo yake husukumwa na maono na mtazamo wa mbali kwa ajili ya binadamu wote na viumbe vyote.Hutazama sio kila kiumbe kwa ajili yake,bali kila kiumbe kwa ajili ya wote.
Anayejitambua habagui jinsia bali hutambua jinsia kuwa ni matokeo ya fikra za Mungu yaliyokusuduia kutoa fursa.Huheshimu, hutambua wengine na kuthamini nafsi zao na uchaguzi wao.Hutengeneza dunia dunia ambayo jinsia zote huwa na uhuru wa kutumia vipawa vyao, kutambua sauti zo,nuru ndani mwao na kutumia kwa ajili ya viumbe wote.
Mtu anayejitambua hasukumwi kutenda na maamuzi ama fikra za wengine. Anatazama ndani yake.Hajifananishi na nafsi zingine na hivyo hatumii nafasi yeyote kuwakandamiza wengine.Husimama kwa miguu yake mwenyewe. Anawasikiliza wengine isipokuwa hatoi nafasi kwa wengine kumuamulia maisha atakayoishi. Anayaona mambo yajayo na hivyo huanza kuijenga kesho yake katika wakati tunaouita sasa. Ni alama ya uwezo wa Mungu uliopo ndani ya binadamu. Na alama ya maisha yake huishi enzi na enzi.
Mtu anayejitambua huchukua hatua juu ya hisia zitokazo ndani mwake na hivyo kutambua matokeo ya matendo yake.Hutenda kwa msukumo wa moyo. Hutambua mambo ambayo hayamletei faida na kutoyafanya na pia hutambua yale yanayomletea faida ..akitambua kuwa anapotenda kwa wengine anajitendea mwenyewe. Husikiliza hisia za ndani mwake na kujifunza lugha ya moyo wake.
Huishi maisha yenye sababu. Husikia muito alioitiwa na kuuuishi. Haridhishwi tu na maisha ya tokanayo na matukio kama kuamka,kutembea,kulala,kula bali hutambua kuwa yupo hapa duniani kwa sababu maalum,hivyo huchimba ndani mwake kuijua sababu na kuiiishi. Kila wakati anasukumwa na sababu hiyo ya yeye kuishi ,kuendelea kuishi kwa dhati akitengeneza na kuifuata njia inayomfikisha huko.
Hakimbii majukumu yake . Hajitoi katika kutafuta suluhu ya changamoto na wala halaumu wengine. Hutambua makosa yake na kujifunza kupitia hayo. Husanifu maisha yake na kuyafanya mapya kila wakati.
Hujifunza toka ndani mwake na kutoka kwa wengine. Hutilia mkazo katika mafanikio ya ukuaji ndani mwake kuliko mafanikio ya nje,hutengeneza ndani mwake. Hutafiti na kuvumbua chemchem zinazojenga na kubomoa nafsi na kutumia chemchem hiyo kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi.Hivyo aliyejitambua ni picha tosha ya uwezo na uwepo wa Mungu ndani ya binadamu. Hutengeneza msawazo kati ya chemchem ndani mwake na matokeo yaonekanayo halisia.
Anayejitambua hatafuti usahihi katika utendaji bali hutenda kwa kujitolea katika nguvu na uwezo wote.Hufanya kwa uwezo wake wote.
Anayejitambua hujikita katika kutenda kuliko kusema tu.Huweka bidii katika kazi. Huanzisha na kutenda mambo ambayo hufaidisha viumbe wote . Husema pale inapohitajika,huheshimu mawazo yake na huwa tayari kuchukua malipo ya maneno yake mwenyewe.Hakimbii kivuli chake. Hayupo tayari kuona wengine wakikosa uhuru kupitia yeye. Anatambua kuwa wakati wote huvuna alichopanda.
Anayejitambua huweka mkazo katika uhusiano mwema na nafsi zingine. Huthamini mahusiano yenye thamani. Mahusiano kwake hutokea ndani, hujengwa ndani na hivyo hudumu. Upendo kwake ni lugha ya moyoni, huleta furaha, mshikamano na amani.Zitokeapo changamoto katika mahusiano,huwa tayari kuyatatua kwa ajili ya kuyakuza zaidi.
Anayejitambua hutambua kuwa hapa duniani hatupo katika kushindana,ushindani kwake haupo,hushirikiana na ushindi kwake ni furaha katika kutimiza wajibu wake. Huandaa silaha zake ndani na kuteketeza kila kisicho na manufaa kwa binadamu. Baada ya milima na mabonde katika maisha yake ushindi huzaliwa ndani mwake. Hutumia uwezo wake kwa ajili ya Wengine na si dhidi ya wengine..
Huishi katika hali ya kujitolea na bidii. Huwa ni zawadi ya aina yake hapa duniani. Haogopi kutenda. Huendeleza mambo yaliyojenga utu,ubinadamu na misingi bora ya kuishi yaliyojengwa na binadamu waliomtangulia. Maisha yake hufundisha wengine. Hutambua juhudi za wengine na wote wanaompa msukumo wa kutenda zaidi hasa pale anapokutana na changamoto. Hutambua kuwa hayuko peke yake,bali dunia imejengwa kwa muungano wa nafsi zinazotimiza majukumu kwa dhati.
Haogopi ukweli hata pale unapoumiza. Hutoa nafasi ya kusamehe kila wakati anapokosewa. Hujisamehe yeye pia anapofanya makosa. Hushiriki katika ujenzi wa maisha yake.
Hutambua kuwa kila jambo hutoa fursa,kila kiumbe ana fursa. Hakusanyi ama kujilimbikizia kwa ajili ya sifa. Hutazama wengine kama anavyofanya kwa nafsi yake. Inapostahili hujitolea alichonacho,hutoa kwa wale walioshiriki kwa yeye kupata. Hutengeneza maisha yake yawe ya kutoa fursa kwa wengine badala ya kuwanyang’anya wengine .
Anayejitambua haichukulii dunia kama chanzo cha maumivu bali hugundua kuwa dunia humpa kila mmoja kadiri anavyohitaji.Dunia husikiliza kutoka kwenye uwezo ulio ndani mwetu tuliopewa na Mungu.Hata mara moja hajichukulii kuwa ni bora kuliko binadamu wengine na wala si dfhaifu kuliko wengine. Hutambua kushabihiana na kutegemeana kati ya kiumbe kimoja na kingine.Hivyo anatambua kuwa kama ikiharibu mazingira,ni sawia na kuharibu nafsi yake.
Ni hayo tu kwa leo.
Kila la heri.
Anayejitambua hatafuti usahihi
katika utendaji bali hutenda kwa kujitolea katika nguvu na uwezo wote.Hufanya
kwa uwezo wake wote.
Anayejitambua hujikita katika kutenda
kuliko kusema tu.Huweka bidii katika kazi . Huanzisha na kutenda mambo ambayo hufaidisha viumbe
wote . Husema pale inapohitajika,huheshimu mawazo yake na huwa tayari kuchukua
malipo ya maneno yake mwenyewe.Hakimbii kivuli chake. Hayupo tayari kuona
wengine wakikosa uhuru kupitia yeye.
Anatambua kuwa wakati wote huvuna alichopanda..
Anayejitambua huweka mkazo katika
uhusiano mwema na nafsi zingine. Huthamini mahusiano yenye thamani. Mahusiano
kwake hutokea ndani, hujengwa ndani na hivyo hudumu. Upendo kwake ni lugha ya
moyoni, huleta furaha, mshikamano na amani.Zitokeapo changamoto katika
mahusiano,huwa tayari kuyatatua kwa ajili ya kuyakuza zaidi.
Anayejitambua hutambua kuwa hapa
duniani hatupo katika kushindana,ushindani kwake haupo,hushirikiana na ushindi
kwake ni furaha katika kutimiza wajibu wake. Huandaa silaha zake ndani na
kuteketeza kila kisicho na manufaa kwa binadamu. Baada ya milima na mabonde
katika maisha yake ushindi huzaliwa ndani mwake. Hutumia uwezo wake kwa ajili
ya Wengine na si dhidi ya wengine..
Huishi katika hali ya kujitolea na
bidii. Huwa ni zawadi ya aina yake hapa duniani. Haogopi kutenda. Huendeleza
mambo yaliyojenga utu,ubinadamu na misingi bora ya kuishi yaliyojengwa na
binadamu waliomtangulia. Maisha yake hufundisha wengine. Hutambua juhudi za wengine na wote wanaompa
msukumo wa kutenda zaidi hasa pale anapokutana na changamoto. Hutambua kuwa hayuko peke
yake,bali dunia imejengwa kwa muungano wa nafsi zinazotimiza majukumu kwa dhati.
Haogopi ukweli hata pale unapoumiza.
Hutoa nafasi ya kusamehe kila wakati anapokosewa. Hujisamehe yeye pia anapofanya
makosa. Hushiriki katika ujenzi wa maisha yake.
Hutambua kuwa kila jambo hutoa
fursa,kila kiumbe ana fursa. Hakusanyi ama kujilimbikizia kwa ajili ya sifa.
Hutazama wengine kama anavyofanya kwa nafsi yake. Inapostahili hujitolea
alichonacho,hutoa kwa wale walioshiriki kwa yeye kupata. Hutengeneza maisha
yake yawe ya kutoa fursa kwa wengine badala ya kuwanyang’anya wengine .
Anayejitambua haichukuliai dunia
kama chanzo cha maumivu bali hugundua kuwa dunia humpa kila mmoja kadiri
anavyohitaji.Dunia husikiliza kutoka kwenye uwezo ulio ndani mwetu tuliopewa na Mungu.Hata mara
moja hajichukulii kuwa ni bora kuliko binadamu wengine na wala si dfhaifu
kuliko wengine. Hutambua kushabihiana na kutegemeana kati ya kiumbe kimoja na
kingine.Hivyo anatambua kuwa kama ikiharibu mazingira ,ni sawia na kuharibu
nafsi yake.
- See more at: http://pongujoseph.blogspot.com/2013/09/sifa-za-binadamu-anayejitambua.html#sthash.2otJTs9x.dpuf
Kamwe
huwezi kufanikiwa kama hujui unachokitaka,huwezi kuona mbele
pasipoonekana kama hufahamu uendapo,ni mpaka pale utakapojua unataka
kuwa nani,ndipo utakapokuwa.....ni sawa na kwenda safari isiyojulikana
hata uelekeo.
Mungu alipokuuumba alikupa nguvu na uwezo,akaifanya dunia na vyote vinavyokuzunguka vitii maagizo yako,hasa yale yanayotokana na msukumo wa moyo wako..hivyo wewe ni kiumbe bora jinsi ulivyoumbwa,wewe ni aidi ya ulivyo,wewe ni upendo,amani,faraja,chuki,visasi,wewe ni mwerevu,na msanifu wa maisha yako mwenyewe,hivyo hupaswi kumlaumu yeyote kuhusiana na jambo lolote linalohusu maisha yako,chukua hatua juu ya maisha yako mwenyewe.
Ndani yako ni chemchemi ya kila hali iletayo matokeo hasi ama chanya,ukifikiri kuhusu upendo utafute ndani yako,ukitaka kujua kuhusu uwezo ulio nao,utafute ndani yako,ukitaka kujua kuhusu mafanikio yako,tafuta ndani mwako...chemchemi yako haileti faida kama hujachukua maamuzi
Huna tofauti na binadamu mwingine kwa maana ya uwezo......anza kwanza kuuchunguza ubora wako uujue,ukiutambua,utambue kuwa wengine ni bora kama wewe,hivyo matendo yako yazingatie matokeo yake,fikra zako ziwe fikra njema juu yako na kwa wengine kwani kila utendalo kwa wengine,umejitendea mwenyewe.Maisha ni uchaguzi wako,na matokeo ya kila unachochagua ni juu yako.
Fikra zitokazo kwako ni sewa na bustani ama shamba,inaitaji kutazamwa na kupaliliwa...kuhakikisha kuwa unapanda mbegu bora,ukipanda mbegu isiyo bora (fikra mbaya dhidi yako na maisha yako) huleta matokeo sawia na mbegu uliyoipanda.
Maisha unayoyaishi hayatokei kwa kiitwacho bahati(nzuri ama mbaya) bali ni matokeo ya uchaguzi wako mwenyewe ama kwa kutambua na kutotambua.Umasikini,utajiri,furaha,huzuni,amani,chuki,upendo vyote ni matokeo ya uchaguzi wa maisha yako.Nguvu na uwezo wa kubadili matokeo hayo hutoka ndani mwako....Ni msukumo utokao ndani mwako pekee ndio utakaobadili maisha yako.
Kamwe wewe huvuti maishani vile vitu unavyovitamani ama maisha unayoyatamani,bali unavuta jinsi ya fikra zako.Fikra a ushindi huleta ushindi,fikra za kushindwa huleta kushindwa.
Mara nyingi unajaribu kubadili hali ama mazingira yanayokuzunguka pasipo kubadili fikra zako juu ya mambo hayo....Jinsi uvitazamavyo vitu huwa...ukilitazama jambo kwa uchanya wake,basi kila hali huwa ni nafasi,kama ni mtazamo hasi,basi matokeo yake huwa hasi na kwako huwa ni maumivu. - See more at: http://pongujoseph.blogspot.com/2012/12/ukweli-kuhusu-wewe.html#sthash.CS8auqKb.dpuf
Mungu alipokuuumba alikupa nguvu na uwezo,akaifanya dunia na vyote vinavyokuzunguka vitii maagizo yako,hasa yale yanayotokana na msukumo wa moyo wako..hivyo wewe ni kiumbe bora jinsi ulivyoumbwa,wewe ni aidi ya ulivyo,wewe ni upendo,amani,faraja,chuki,visasi,wewe ni mwerevu,na msanifu wa maisha yako mwenyewe,hivyo hupaswi kumlaumu yeyote kuhusiana na jambo lolote linalohusu maisha yako,chukua hatua juu ya maisha yako mwenyewe.
Ndani yako ni chemchemi ya kila hali iletayo matokeo hasi ama chanya,ukifikiri kuhusu upendo utafute ndani yako,ukitaka kujua kuhusu uwezo ulio nao,utafute ndani yako,ukitaka kujua kuhusu mafanikio yako,tafuta ndani mwako...chemchemi yako haileti faida kama hujachukua maamuzi
Huna tofauti na binadamu mwingine kwa maana ya uwezo......anza kwanza kuuchunguza ubora wako uujue,ukiutambua,utambue kuwa wengine ni bora kama wewe,hivyo matendo yako yazingatie matokeo yake,fikra zako ziwe fikra njema juu yako na kwa wengine kwani kila utendalo kwa wengine,umejitendea mwenyewe.Maisha ni uchaguzi wako,na matokeo ya kila unachochagua ni juu yako.
Fikra zitokazo kwako ni sewa na bustani ama shamba,inaitaji kutazamwa na kupaliliwa...kuhakikisha kuwa unapanda mbegu bora,ukipanda mbegu isiyo bora (fikra mbaya dhidi yako na maisha yako) huleta matokeo sawia na mbegu uliyoipanda.
Maisha unayoyaishi hayatokei kwa kiitwacho bahati(nzuri ama mbaya) bali ni matokeo ya uchaguzi wako mwenyewe ama kwa kutambua na kutotambua.Umasikini,utajiri,furaha,huzuni,amani,chuki,upendo vyote ni matokeo ya uchaguzi wa maisha yako.Nguvu na uwezo wa kubadili matokeo hayo hutoka ndani mwako....Ni msukumo utokao ndani mwako pekee ndio utakaobadili maisha yako.
Kamwe wewe huvuti maishani vile vitu unavyovitamani ama maisha unayoyatamani,bali unavuta jinsi ya fikra zako.Fikra a ushindi huleta ushindi,fikra za kushindwa huleta kushindwa.
Mara nyingi unajaribu kubadili hali ama mazingira yanayokuzunguka pasipo kubadili fikra zako juu ya mambo hayo....Jinsi uvitazamavyo vitu huwa...ukilitazama jambo kwa uchanya wake,basi kila hali huwa ni nafasi,kama ni mtazamo hasi,basi matokeo yake huwa hasi na kwako huwa ni maumivu. - See more at: http://pongujoseph.blogspot.com/2012/12/ukweli-kuhusu-wewe.html#sthash.CS8auqKb.dpuf
No comments:
Post a Comment