TUTU AMSIHI MUSEVENI KUHUSU MUSWADA MPYA
Askofu mstaafu wa Cape Town, Desmond Tutu, amemsihi
Rais Museveni wa Uganda asitie saini mswada ulioleta utatanishi kuhusu
wapenzi wa jinsia moja.
Askofu Tutu, aliyewahi kupata tuzo ya amani ya
Nobel, alisema amevunjika moyo kuwa Rais Yoweri Museveni anaonesha
kubadilisha msimamo wake, kwa vile awali alisema kuwa hataruhusu mswada
huo kuwa sheria.
Desmond Tutu alisema haistahiki kuwa na ubaguzi
kama huo, na alitoa mifano ya mfumo wa zamani wa ubaguzi wa rangi
uliokuwako Afrika Kusini na ubaguzi wa Wa-Nazi wa Ujerumani.
Alisema hiyo ni mifano mibaya kabisa.
Awali mswada wa Uganda ulipendekeza kifo kwa vitendo vya kulawiti na baadae kubadilishwa kuwa adhabu ya kifungo.
No comments:
Post a Comment