JINSI YA KUKABILIANA NA UGUMU WA MAISHA
Maisha ni magumu kwa Watanzania wengi na mbaya zaidi bei za bidhaa mbalimbali zinapanda kila siku na pesa haionekani inakopotelea kutokana na matumizi mbalimbali ya familia kua juu.
Mbinu za kuyakabili maisha hazijabadilika tangu zama hizo hela ianze
kutafutwa: tafuta pesa, bana matumizi, hifadhi ziada, na wekeza kwa
umakini.
Ili kufanikisha hayo jitahidi kufanya yafuatayo:-
1.Punguza matumizi yasiyo ya lazima, mf. kunywa soda au bia nyingi kwa siku, kutoa ofa zisizo
na msingi, kununua vyakula kwenye mighahawa wakati unaweza kupata
ofisini au nyumbani, kula ovyo barabarani (pipi, karanga, ..) hata
kama huna njaa.
2. Fanya tathmini juu ya bei nafuu na upatikanaji wa bidhaa bora. Andaa
orodha ya vitu unavyotaka kununua kabla hujaenda sokoni/dukani/ jitahidi kufuata orodha yako tuu.
Usinunue usichopanga. Pia tunza kumbukumbu za manunuzi yako hii itakuwezesha kufanya tathmini wakati wa kutaka kuondoa
baadhi ya vitu ambavyo havikuwa vya lazima.
3. Punguza matumizi ya umeme na maji mfano kutokuacha redio au tv inawaka siku
nzima, laptop kwenye charge wakati hautumii, kutengeneza bomba za maji
zinazovuja, kuoga kwa kutumia shower, sambamba na kuoga haraka si lazima
utumia dk 30 bafuni.
4. Punguza matumizi ya simu kwa kutokupiga simu zisizo na ulazima.
Unaweza kujiunga na vifurushi vya gharama nafuu kwa siku/wiki hata
mwezi na endapo hakuna ulazima usijiunge.
5. Punguza safari zisizo na tija, Kwa wenye magari, unaweza kutumia
usafiri wa daladala kwenda sehemu panapofikika kwa urahisi. Pia, tembea
kwa miguu ukiwa mitaani, punguza gharama za mafuta kwa kuendesha
taratibu.
6. Punguza starehe zinazogharimu. Mf. kwenda sehemu
za kifahari (bia 1 - 4,000), kuhudhuria tafrija au sherehe zisizokulazimu.
7. Nunua vyakula (unga, sukari, ..) kwa bei ya jumla sokoni na kuhifadhi
nyumbani hususani visivyoharibika, kwa vinavyoaharibika, nunua kiasi
visije kuharibika na vipikwe kwa kiasi
kinachotosha wakati husika, na kikibaki hifadhi (usitupe chakula wala usisaze), unaweza kwenda
ofisini na lunch box.
8. Nunua sabuni za jumla dukani, natumia kwa uangalifu. Kiasi kidogo cha
sabuni za kufulia na kuogea kinatosha. Nunua bidhaa (manukato,
nguo, viatu,..) utakazokua unatumia tuu, mf. kuna watu wana aina kadhaa za
perfume ambazao ni za gharama. Kununua vitu na kukihifadhi haina maana na ni
upotezaji wa pesa.
9. Jiunge kwenye bima mbalimbali endapo hali inaruhusu. Mf. Bima za afya, maisha, nyumba,
gari, zenye manufaa kwako, na fanya uchunguzi kabla ya yote, bila
kusahau mifuko ya akiba.
10. Lipa bili zako kwa wakati, bila kusahau madeni uliyokopa kwa watu.
Ukiona unazidishiwa gharama kwenye bili zako uliza. Epuka kulipia kitu
ambacho hujatumia kwa uhalali.
12. Epuka kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao labda itokee dharura. Kwa mfano, kununua muda
wa maongezi kutoka benki, credit card, kulipia huduma kwa kadi za benki.
Lipa kwa fedha
taslimu uone thamani na maumivu ya kutoa pesa.
13. Unapoona fursa yoyote itakayokupunguzia gharama itumie ipasavyo. Mf.
punguzo la bei, mnada na usisite kuomba punguzo la bei.
14. Fungua akaunti mbili benki, akaunti ya matumizi na kaunti ya
kukusanyia mtaji wa uwekezaji. Ili kupunguza gharama, kaunti zote
zisiwe gharama za uendeshaji i.e makato ya mwezi (hususani akaunti ya
kukusanyia fedha za uwekezaji). Hakikisha kila mara unaweka kiasi
cha fedha kwenye akaunti hizo. Katika kila mapato yako, weka angalau asilimia 20 katika akaunti ya uwekezaji.
16. Wekeza pesa uliyokusanya katika mradi wowote ili kujiongezea kipato.
Usifanye biashara bila malengo au kuiga kutoka kwa marafiki.
17. Saidia wahitaji. Kujigharamia peke si sehemu ya maadaili katika
jamii yoyote ile! Jitahidi kutoa msaada kwa watu wanohitaji kwa dhati
msaada kutoka kwako. Mfano, kuwasaidia yatima, wagonjwa wasio na msaada,
kutembelea wazee. Kufanya hivyo kutafupa faraja ya kweli, na
watakuombea upate baraka zaidi.
18. Unaweza kuotesha miche kadhaa ya nyanya miongoni
mwa maua yako ya nyumbani, kuotesha miti ya matunda itakayokupatia
kivuli na matunda, minazi. Usikubali kuotesha mimea yenye faida moja tu,
mf. mapambo au kivuli, nyumbani kwako.
N.B:
Kuwa makini usiwe bahili, yaani, kubana matumizi pasipo sababu ya msingi. Huwezi kufurahi maishani kwa kujinyima kupita kiasi.
No comments:
Post a Comment