BUNGE LA UKRAINE KUJADILI SERIKALI MPYA
Maelfu ya waandamanaji wameendelea na maandamano
katikati ya mji wa Kiev wakati Wabunge wakikutana kujadili kuhusu
uundwaji wa Serikali mpya nchini Ukraine.
Hali katika viwanja vya uhuru imetulia, ikiwa ni
siku moja baada ya Bunge kupiga kura kumuondoa Rais wa nchi hiyo,
Viktor Yanukovych,hatua ambayo amedai kuwa ni mapinduzi huku mpaka sasa
akiwa hajulikani alipo.
Mpinzani wake mkuu, Waziri mkuu wa zamani Yulia
Tymoshenko, pia aliachiwa huru toka kifungoni , hatua hii imekuja baada
ya maandamano dhidi ya Serikali ya nchi hiyo yaliyodumu kwa miezi
kadhaa.
Yulia tymoshenko alihukumiwa kifungo cha miaka
saba jela akishutumiwa kutumia vibaya madaraka yake, na kuachiwa kwake
yalikua madai ya msingi ya waandamanaji nchini humo.
Wabunge wa upinzani wameiambia Televisheni ya
taifa kuwa Bunge litajadili kuhusu uundwaji wa Baraza jipya la mawaziri
na uteuzi wa Waziri mkuu.
No comments:
Post a Comment