ARSENAL YAIKUNG'UTA LIVERPOOL 2-1
Washika bunduki kutoka jiji la London maarufu kama ''The Gunners'' jana waliitandika timu ya Liverpool jumla ya magoli 2-1 katika mchezo wa kombe la FA na kujihakikishia kutinga hatua ya robo fainali za kombe hilo.
Arsenal ilipigwa jumla ya magoli 5-1 mara ya mwisho ilivyokutana na timu hiyo katika mtanange wa ligi kuu ya Uingereza; hivyo jana ililipa kisasi na kuwatoa Liverpool katika kinyang'anyiro cha kombe hilo.
Goli la kwanza la Arsenal lilifungwa na Oxlade-Chamberlain katika dakika ya 16 ya mwanzo wa mchezowakati goli la pili likifungwa na Lukas Podolski na baadae timu ya Liverpool ilipata goli kwa njia ya Penati kupitia kiungo wake Steven Gerrard.
Japokuwa Mwamuzi wa mchezo huo '' Howard Webb'' ambaye atachezesha baadhi ya michezo ya kombe la dunia mwaka huu; alionekana tupowapa Liverpool penati ya wazi baada ya mshambuliaji wake Luis Suarez kuchezewa rafu mbaya ndani ya dimba la Arsenal na Oxlade-Chamberlain wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment