ZIMBABWE: Chama cha ZANU PF kuchangisha pesa kwaajili ya siku ya kuzaliwa ya raisi Mugabe
Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe
CHAMA tawala nchini
Zimbabwe Zanu-PF, kinapanga kuchangisha kiasi cha zaidi ya Sh85 milioni
kwa ajili ya sherehe maalumu ya siku ya kuzaliwa kwa kiongozi wa nchi
hiyo Robert Mugabe, ambaye atakuwa anaadhimisha miaka 90 mnamo Februari
21.
Rais Mugabe amekuwa kiongozi wa zimbabwe tangu ijinyakulie uhuru wake miaka 34 iliyopita.
“Hizi ni
sherehe za kipekee, kuadhimisha miaka 90 siyo rahisi,” akasema Bw Absalom
Sikhosana, katibu wa masuala ya vijana wa chama cha Zanu-PF.
Sherehe hiyo ya aina yake inatarajiwa kufanyika Februari 23 katika mji wa Marondera.
Bw Sikhosana
alisema kundi la vijana wa Zanu-PF ndilo limepewa jukumu la kuandaa
sherehe hizo na wanalega kuchagisha kiasi cha kati ya dola $700,000 na
$1milioni.
Hiyo
haitakuwa mara ya kwanza kwa Zimbabwe, ambayo ni miongoni mwa mataifa
masikini duniani, kutumia mamilioni ya fedha katika sherehe zinazomhusu
Rais Mugabe.
No comments:
Post a Comment