Friday 23 May 2014


 

 WANANCHI WAMLIPUA LISSU KWA KINANA


Wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki, wamemuomba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, awasaidie kutatua kero zinazowakabili za barabara, elimu na afya.

Wananchi hao wamedai hatua ya kumuomba Kinana awasaidie inatokana na Mbunge wao, Tundu Lissu (Chadema), kuwakataza kuchangia miradi ya maendeleo hali iliyosababisha miradi ya ujenzi wa shule na zahanati kusimama kwa kipindi cha miaka minne.

Wakizungumza jana wilayani Ikungi mkoani Singida, mbele ya Kinana, wananchi hao walisema Mbunge huyo amekuwa akiwakataza kuchanga fedha kwa ajili ya kujenga madarasa na majengo ya zahanati kwa madai kuwa serikali ina fedha za kutosha za kufanya kazi hizo.

“Ndugu Kinana tunaomba utusaidie kwani tangu tulipomchagua Mbunge wetu, Tundu Lissu, hajaendeleza miradi ambayo ilianza kufanywa na Mbunge wa CCM aliyepita, baada ya yeye kutukataza kuchanga aina yeyote ya michango itakayotakiwa na halmashauri kwa ajili ya maendeleo, tumeendelea kuwa katika hali ya ufukara” alisema Omary Lissu mkazi wa kijiji cha Unyanghumpi.

Alisema tangu wamekatazwa kutoa fedha za miradi hakuna kazi ambayo imeendelea hasa katika zahanati Kimbwi ambayo walitarajia iwe imeanza kutumika tangu mwaka 2011 lakini hadi sasa bado haijakamilika na kwamba diwani wao amekuwa akiwashinikiza kutoshiriki shughuli hizo.

Naye Mwalimu wa Shule ya Msingi Unyanghumpi, Juliana Joseph, ambaye anafundisha darasa la awali, alisema tangu madarasa hayo yajengwe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, mpaka sasa hakuna majengo mengine mapya wala ya zamani kumaliziwa hali inayowafanya baadhi ya wanafunzi kusoma katika darasa ambalo halijaezekwa.

“Ni mwaka wa nne nafundisha katika darasa hili ambalo halina paa,  na mvua inaponyesha inatubidi tusiudhurie vipindi. Mbunge wetu na diwani walitoa tamko la kuwataka wananchi wasichangie umaliziaji wa jengo ndiyo maana hadi sasa tuko hapa, wala hajawahi kufika kutoa msaada wowote,” alisema Joseph.

Alisema darasa la awali lina jumla ya wanafunzi 135 ambao wote wanakaa kwenye vumbi kwani hakuna madawati na vifaa vingine kama dhana za kufundishia. Mkazi mwingine alisema wamekuwa wakipata tabu ya kufuata huduma ya afya katika kijiji kingine wakati kijijini hapo kuna zahanati ambayo imejengwa inasubiri kukamilika.

Akizungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Makyungi, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kiongozi bora ni yule anayechangia maendeleo ya wananchi na siyo kuwakataza wananchi kufanya maendeleo.

Alisema Tundu lissu anafanya mambo ambayo hayaendani na matarajio ya wananchi kwani walimchagua wakiamini ataleta maendeleo badala yake anazuia maendeleo. Kwa upande wake, Kinana, alimtaka Lissu kuacha porojo za majukwaani na arudi kwa wananchi kuwatimizia ahadi alizotoa kwani anafedha nyingi anazopatiwa bungeni.

Alisema wilaya ya Ikungi iko nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na wilaya nyingine nchini sababu kubwa ikiwa ni mbunge mwenyewe ambaye ameshindwa kupigania maendeleo ya jimbo lake na badala yake amekuwa akigombana na kila mtu serika
lini.

  UN YASEMA VATCAN INAPUUZA HAKI ZA WATOTO


 PAPA FRANCIS

Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi mateso imelaumu vikali kanisa Catholiki kwa kutoshughulikia ipasavyo suala la unyanyasaji wa watoto ndani ya kanisa hilo.
Katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni na Umoja huo mjini Geneva , Kamati hiyo imeushutumu utawala wa Vatcan kwa kuwahamisha watawa kutoka parokia moja hadi nyingine kuwaepusha kushtakiwa, na kupuuza haki za waathiriwa za kupokea fidia .
Utawala wa Vatican uliithinisha mkataba dhidi ya unyanyasaji , ukatili na matendo yaliyo kinyume na utu.Uchunguzi uliofanywa na kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Vatcan ni sehemu ya uchunguzi wa mara kwa mara wa kamati hiyo dhidi ya nchi wanachama ili kuhakikisha mikataba inatekelezwa.

Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa ina hofu kuwa wakati utawala wa Vatcan umeelezea kutokubali kamwe kuwepo kwa unyanyasaji ndani ya kanisa, maneno hayaendani na vitendo .

Kamati hiyo imekasirishwa zaidi na kwamba Utawala wa Vatcan unasisitiza kuwa unahusika zaidi na wahudumu wanaofanyika kazi ndani ya Vatcan kwenyewe , kuliko makasisi wake wanaofanyika kazi kwingineko duniani.

Mwezi Januari mwaka huu utawala wa Vatcan ulichunguzwa upya na kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto, baada ya kupokea ukosoaji kama huo kwamba ulishindwa kuwalinda watoto waliokuwa chini ya uangalizi wake.

 GERMAIN KATANGA JELA MIAKA 12

Germain Katanga

Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC imemhukumu kiongozi wa zamani wa wanamgambo waasi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Germain Katanga, kifungo cha miaka kumi na miwili jela baada ya kumpata na hatia ya uhalifu wa kivita. 
 
Bwana Katanga alipatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji ya mamia ya wanavijiji katikaeneo la Ituri Katanga mwezi Machi mwaka 2003.

Jimbo la Katanga ni jimbo lenye utajiri wa madini ya dhahabu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo . Lakini kiongozi huyo wa waasi mwenye umri wa miaka thelathini na sita hakupatikana na hatia ya kuwatumikisha watoto vitani na makosa mengine ya ubakaji.