Wednesday, 12 February 2014



AFRIKA KUSINI: WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA



http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/b7e45d3a06b99bee20ce4fa12b57697c_XL.jpg



Waafrika Kusini zaidi ya millioni ishirini na tano na pointi tatu (25.3) wameweka rekodi nchini Afrika ya kusini kwa kujiandikisha kwa wingi kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi ujao huku kukiwa na ongezeko la watu milioni moja katika wiki iliyopita.

Uchaguzi mkuu ujao ambao unatarajiwa kufanyika mnamo mwezi Mei mwaka huu 2014, huku wengine milioni moja wakijiandikisha mwishoni mwa wiki iliyomalizika. Hayo yameripotiwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.
Kiwango hicho cha uandikishaji wa wapiga kura kimepanda kutoka asilimia 76.9 wiki iliyopita na kufikia asilimia 80. 5 hapo jana.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini kutoka chama tawala cha Afrika National Congress (ANC) ambacho kimekuwa madarakani kwa miongo miwili, amekuwa akikosolewa na kukabiliwa na upinzani kutokana na kuongezeka umaskini na ukosefu wa ajira nchini humo. Hata hivyo utabiri unaonyesha kuwa chama cha ANC kinaweza kuibuka na ushindi katika uchaguzi ujao licha ya kukabiliwa na changamoto hizo kutoka na kua na watu wengi wanaokiunga mkono.

No comments:

Post a Comment