Tuesday, 18 February 2014

 WACHIMBAJI MADINI MIGODINI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

save_240df.jpg

Kundi la wachimbaji madini katika migodi haramu waliookolewa kutoka mgodi uliotelekezwa nchini Afrika Kusini na maafisa wa uokoaji wanatarajiwa kufika kizimbani hivi leo.
Wachimbaji  hao 11 walitumia ngazi iliyotupwa ndani ya mugodi huo kujinasua siku ya jumatatu.
Wote 22 walikamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Vyombo vya habari vya Afrika Kusini vinasema takriban wachimbaji wengine 200 bado wamenasa katika mgodi huo lakini wamekataa kuokolewa wakihofia kukamatwa na polisi. Baadhi yao wanatoka katika mataifa jirani.

No comments:

Post a Comment