Tuesday, 18 February 2014

MWANASHERIA ASEMA BUNGE LA KATIBA HALITABADILI RASIMU



Wananchi wameondolewa hofu kwamba wajumbe wa Bunge la Katiba kazi yao haitakuwa kubadili maoni yao yaliyomo katika rasimu ya katiba bali kufanya uchambuzi wa mapendekezo yaliyopo.
 
 

Akizungumza katika Kongamano la rasimu ya pili ya katiba, lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Teku.Mwana sheria wa Jiji la Mbeya, Chrispin Kaijage, alisema  wananchi wasiwe na wasiwasi kwa kuwa wajumbe  kazi yao itakuwa ni kufanya uchambuzi.

Alisema wananchi wasiwe na wasiwasi kwa kuwa maoni waliyoyatoa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba hayatabadilishwa.

Alisema kazi ya Bunge itakuwa ni kuchambua rasimu hiyo ya pili na kuwa wataongeza vitu vichache ambavyo vitaondokana kuna haja ya kuongezwa.

Alisema kuwa katika bunge hilo kuna wanasheria wengi wenye upeo mkubwa wa kisheria na kwamba pia kuna watu kutoka katika taasisi mbalimbali katika jamii.

Alisema kuwa kongamano liliandaliwa kufanya uchambuzi wa mambo ambayo yapo katika katiba hiyo na kuongeza vitu ambavyo wanaona kuwa vinapaswa vitaongezwa katika katiba mpya.

Aliwaondoa wasiwasi wananchi kwa kuwa rasimu hiyo itarudishwa kwao ili waipigie kura ya maoni.

No comments:

Post a Comment