CHADEMA YATISHIA KUSUSIA BUNGE
Zikiwa zimebaki siku nne kabla ya kuanza kwa Bunge la Katiba mjini Dodoma, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitasusia bunge hilo, iwapo mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Jaji Warioba hayatazingatiwa.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakati alipokuwa akitoa taarifa ya
Mkutano wa Kamati Kuu ya chama hicho uliofanyika juzi, kuzungumzia Bunge
la Katiba, uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga na uamuzi kuhusu
madiwani wake mkoani Arusha.
Mbowe alisema Chadema wanakwenda kushiriki bunge
hilo wakiwa na masikitiko kwa kuwa uteuzi wa wajumbe 201 uliofanywa na
Rais Jakaya Kikwete haukuwa na nia njema kwa taifa, kwani asilimia 80 ya
walioteuliwa ni wanachama wa CCM.
“Tunakwenda Dodoma lakini hatutakubali Bunge limilikiwe na wachache na hatutasita kurudi kwa wananchi tutakapoona mapendekezo ya Jaji Warioba hayatekelezwi,” alisema Mbowe.
“Tunakwenda Dodoma lakini hatutakubali Bunge limilikiwe na wachache na hatutasita kurudi kwa wananchi tutakapoona mapendekezo ya Jaji Warioba hayatekelezwi,” alisema Mbowe.
Aliongeza kuwa Chadema hawaendi bungeni kugoma ila
wananchi wasishangae watakapoona wanatoka ndani ya Ukumbi wa Bunge
hilo, kwa kuwa lengo la uteuzi wa wajumbe lilikuwa ni kutaka kupata
wabunge wengi watakao unga mkono CCM.
“Kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano, CCM tayari
wana wajumbe karibu asilimia 80, katika Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar wana wajumbe karibu asilimia 68, kwa hiyo wanaweza wakakidhi
vigezo vya mshindi kupatikana kwa theluthi mbili ya kura zilizopigwa
kufanya uamuzi kwa niaba ya Bunge la Katiba,” alisema Mbowe.
Hata hivyo, alisema Chadema hakitajali maoni
yatakayotolewa na CCM ikiwa yatazingatia maoni yaliyotolewa na Tume ya
Jaji Warioba.
“Tutafanya kazi na wajumbe wote walioteuliwa na
Rais, hatutawabagua kwasababu wametokea vyama gani, hapana, ila
tunachokitahadharisha ni kwamba wajumbe wote wataweka masuala ya taifa
mbele na hawataendekezwa na itikadi za vyama vyao.
No comments:
Post a Comment