Tuesday, 11 February 2014

HUKUMU YA VIGOGO TBA: Jela miaka 9 au faini



 






























Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA, Makumba Kimweri na mwenzake wamehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela au kulipa faini ya sh. milioni 15 kila mmoja.
 

Washitakiwa hao wametiwa hatiani kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kutoa kibali cha ujenzi wa ghorofa 18 mtaa wa Chimara Dar es Salaam jirani na Ikulu kitalu namba 45 na 46 kinyume cha sheria.

 

Kimweri  mwenye umri wa miaka 60 na aliyekuwa Msanifu Mkuu wa TBA Richard Maliyaga umri miaka 55 wote wakazi wa jijini Dar es Salaam,walihukumiwa adhabu hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu walinusurika kwenda jela baada ya kulipa faini hiyo.

Hukumu ilisomwa na aliyekuwa Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Sundi Fimbo aliyesikiliza shauri hilo. Kwa sasa amehamishiwa katika mahakama hiyo.

No comments:

Post a Comment