Saturday, 8 February 2014

NAPE NNAUYE: "KUWAZUIA WATU KUPIGA KURA NI KUHUJUMU DEMOKRASIA"


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliyasema hayo wakati akihutubia wakazi wa kata ya Nyasura wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani ambapo aliwaeleza wananchi.Nnauye alifafanua zaidi kua haikuwa rahisi kuwaleta watanzania pamoja,hivyo basi wakatae kabisa vyama viinavyotaka kuwatenganisha kwa misingi ya udini na ukabila.

Nape Nnauye ambaye aliwaambia wananchi waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni za udiwani zinazoendelea nchi nzima ambapo kata 27 zitafany uchaguzi wa madiwani. Alitanabaisha kwamba safari hii CCM haipo tayari kuhujumiwa na kutaka watu wengi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na kutoa wito kwa vijana kulinda wapiga kura wa CCM.



Mgombea wa Udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Nyasura  Ndugu Alexander Mwikwabe akiomba kura toka kwa wananchi wa kata ya Nyasura kwenye mkutano wa hadhara  ambapo mgeni wa heshima alikuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye tarehe 7 mwezi wa pili 2014.

No comments:

Post a Comment