Saturday 28 June 2014

 MAKAMU WA RAISI ALGENTINA ASHITAKIWA


 


Makamu wa raisi nchini Argentina Amado Boudou ameshitakiwa na shitaka la ufisadi.

Bwana Badou anashutumiwa kwa kutumia vibaya mamlaka wakati alipokuwa waziri wa uchumi alipochukua umiliki wa kampuni inayochapisha fedha za Argentina.

Washitakiwa wengine watano pia wameshitakiwa kwa kosa hilo .
Bwana boudou kwa mara kadhaa amepinga mshtaka dhidi yake huku akifutilia mbali wito wa kujiuzulu.Kwa sasa yuko katika ziara ya kibiashara nchini Cuba.

Monday 23 June 2014

WAANDISHI AL JAZEERA WAHUKUMIWA MIAKA 7 JELA



Mahakama nchini Misri imewahukumu jela miaka saba wandishi watatu wa habari wa shirika la habari la Al Jazeera waliokuwa wamezuiliwa kwa miezi sita nchini humo.
Walipatikana na hatia ya kueneza habari za kupotosha na kushirikiana na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Muslim Brotherhood.
Mmoja wa wandishi hao ni Peter Greste, raia wa Australia na ambaye pia alikuwa mwandihi wa habari wa BBC wakati moja.
Hukumu ilipotolewa, Greste kwa hasira aligonga mkono wake katika eneo ambako walikuwa wamezuiliwa huku mwenzake akibururwa kutoka mahakamani na walinzi wa gerezani.

Familia za watuhumiwa nao wakaangua kilio. Kesi hii imelaaniwa sana kote duniani hasa na mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na mashirika ya habari ya kimataifa.
Lakini nchini Misri, vyombo vya habari vilipeperusha habari hiyo kwa utofauti mkubwa.

Al Jazeera - ni shirika linaloonekana kuunga mkono vuguvugu haramu la Muslim Brotherhood na kwa mtanzamo huo , ni adui wa serikali.
Peter Greste ,ndiye alikuwa anaripoti matukio nchini Misri Disemba mwaka jana wakati wa harakati za mapinduzi.

Kisha yeye na wenzake wawili wakatuhumiwa kwa kusaidia vuguvugu la kigaidi na kutangaza taarifa za kupotosha dhidi ya serikali na maslahi ya taifa hilo.
Madai ambayo serikali ya Australia imekuwa ikikanusha vikali.

Serikali ya Australia ilitoa taarifa yake ikisema kuwa imeshtushwa sana na uamuzi wa mahakama katika kesi ya Peter Greste. Imeelezea kushangazwa sana na hukumu iliyotolewa. Serikali imesema haielewi kabisa matukio haya.

Shirika la Al Jazeera lenyewe limepinga hukumu iliyotolewa dhidi ya wandishi hao, Peter Greste, Mohamed Fahmy na Baher Mohamed likisema kuwa inakiuka sheria.

TAASISI YA AFYA YASHAMBULIWA NIGERIA


Mlipuko umeripotiwa kutokea katika taasisi moja ya umma ya mafunzo ya afya katika mji wa Kano ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria.

Duru zinasema kuwa idadi ya watu waliojeruhiwa katika shambulizi hilo dhidi ya kituo cha mafunzo ya afya , bado haijulikani.
Mji huo umewahi kulengwa na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram, ambao wanataka kubuniwe taifa la kiisilamu Kaskazini mwa Nigeria.

Majimbo matatu Kaskazini mwa Nigeria bado yapo chini ya sheria ya hali ya hatari kufuatia miaka mingi ya harakati za wapiganaji hao wa kiisilamu.