YANGA YAWACHAPA WACOMORRO 7-0
Mrisho Ngassa
Mshambuliaji
wa Yanga Mrisho Ngassa leo ameipatia timu ya Yanga ushindi mnono dhidi ya Wacomorro. Ngassa aliziona nyavu za wacomorro kwa mara ya kwanza baada ya kuruka na kupiga mpira wa kichwa na kufunga bao
la kwanza katika dakika ya 13 kipindi cha kwanza.
Katika mchezo huo wa
Klabu Bingwa Barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Komorozine ya Comorro,
uliomalizika mda mfupi uliopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 7-0.
Yanga na Komorozine wakilisakata kabumbumbu
Ngassa
alipachika mabao matatu kati ya saba katika dakika za 13, 64 na 68. Bao
la pili lilifungwa na Nadir Haroub, katika dakika ya 16, Didier
Kavumbagu, dakika ya 57 na 80 na Hamis Kiiza, akifunga bao katika dakika ya 59.Katika mchezo huu wa leo wacomorro walijikuta wakimsindikiza Ngasa akichanja mbuga hadi nyavuni kwao na kumshuhudia akipachika bao mbele ya macho yao.Kwa ushindi huu yanga wamesema watapeleka timu B katika mechi ya marudiano.
No comments:
Post a Comment