MAKAO MAKUU YA CHADEMA YANUSURIKA KUUNGUA MOTO
Makao makuu ya chama cha demokrasia na maendelea Chadema yaliyopo
jijini Dar es salaam yamenusurika kuteketea kwa moto baada ya watu
wasiojulikana kufanya jaribio la kulipua makao hayo usiku wa kuamkia jana
tarehe 11 2014.
Waandishi waliofika katika makao makuu ya
chama hicho na kushuhudia askari wa upelelezi wakiendelea na hatua za
awali za upelelezi huku katibu mkuu wa chama hicho Docta Wilbrodi Slaa
akilaani kitendo hicho na kutaja tukio hilo ni mwendelezo wa
matukio ambayo yamekuwa yakikikumba chama hicho na kuitaka serikiali
kuwa makini na vitendo hivyo kwani vinaweza kuchangia upotevu wa amani
hapa nchini.
Aidha Dr Slaa pia amefafanua kauli yake aliyowahi kuitoa kwa rais Kikwete kuwa kama hata ingilia kati vitendo hivyo nchi haita tawalika kwani itafikia kipindi vitendo kama hivyo havitavumiliwa miongoni mwa Watanzania na kuitaka serikali iingilie kati ili wale wote wanaoendelea kufanya vitendo hivyo wawezea kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

No comments:
Post a Comment