ASASI DRC ZATAKA AL BASHIRI AKAMATWE
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu katika
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, yamesema kuwa Serikali ya nchi
hiyo itachukuliwa kuwa dhaifu iwapo hawamkamati Rais wa Sudan, Omar el
Bashir.
Mashirika yapatayo 90 yalitoa wito Serikali ya
DRC imkamate el Bashir ambaye alikuwa mjini Kinshasa kushiriki katika
vikao vya muungano wa COMESA.
Mmoja wa waandalizi wa maandamano ya
kushinikiza Serikali imkamate kiongozi huyo wa Khartoum, Bwana Andre
Kito Masimango, amesema:
"kuna barua ambayo inasema kuwa mahali po pote
ambapo El Bashiri anapatikana anapaswa kukamatwa na kupelekwa kwenye
mahakama ya kimataifa."
Mkerektwa huyo wa haki za kibinadamu anasema
kuwa Rais El Bashir anapaswa kukamatwa kwa heshina ya waathirika wa
dhuluma inayodaiwa kufanywa nchini Sudan na hata DRC yenyewe.
Watu kadhaa ambao wametoa maoni kwenye mtandao
wa BBC wamesema kuwa lilikuwa kosa kwa Serikali ya DRC kumkaribisha Rais
El Bashar kwa mkutano wa COMESA huku ikijua kuwa anatafutwa.
Hata hivyo kuna wale wanaosema kuwa msimamo wa
Umoja wa Afrika (AU) ambao unasema kiongozi anayetawala hapaswi
kukamatwa unapaswa kuzingatiwa ili El Bashir asikamatwe ugenini DRC.
No comments:
Post a Comment