Wednesday, 19 February 2014

FAIDA ZA KITUNGUU MWILINI

 FAIDA ZA KITUNGUU MAJI MWILINI

 
Kitunguu ni aina ya mboga ya jamii ya yungiyungi . Ni mboga yenye harufu kali inayochangamsha  na kinatakiwa kutumika kikiwa kibichi mara baada ya kukikata.
Imethibitishwa kisayansi kuwa juice yake huuwa vijidudu vya kinamasi na vya kifua kikuu, vijidudu hufa mara tu baada ya kunusa moshi wake.
Imethibitishwa kuwa kwenye kitunguu kuna viuaji sumu vyenye nguvu zaidi ya penisilin(penicillin)na pia ndani yake inapatikana  vitamin C.
Kutokana na utafiti huo umeonyesha kuwa tukitumia vitunguu vibichi mbali na kuongeza kinga za mwili pia hutibu maradhi  yote yatokanayo na bakteria na pia huimarisha misuli ya mwili mara unavuta moshi wake.
Baadhi ya maradhi yaliyodhibitishwa kikinga na kutibiwa na vitunguu ni pamoja na:-
- uvimbe wa mapafu(pneumonia)
- kukojoa kwa kupata maumivu
- Pumu  
- Vidonda vya tumbo
- Saratani
- Kisukari
- Kifua kikuu
- Huongeza hamau ya kula
- Hulainisha chakula tumboni.
Kwa ukweli huo tunashauriwa kujenga tabia ya  kutumia vitunguu  vibichi hata ikiwezekana kila siku. tujitahidi kwani ni mboga ambayo inapakitikana kwa urahisi na tunaitumia kila siku katika vyakula vyetu ingawaje mara nyingi tunavichanganya katika mboga kwa kuvipika,sasa tujitahidi kuwa tunavitumia vikiwa vibichi katika milo yetu ili tuweze kujenga kinga za miili yetu  na kuwa wenye nguvu na afya  njema.

1 comment: