CCM YASHINDA KWA KISHINDO IRINGA:Uchaguzi mdogo wa Madiwani.
wananchi wakifurahia ushindi
Taarifa zaidi inasema kua wananchi wameshiriki kikamilifu katika uchaguzi huo na kupelekea kukipatia Chama cha Mapinduzi ushindi huo mnono kufuatia kufariki dunia kwa madiwani waliokua madarakani na kuacha nafasi hizo wazi.
wananchi wakifurahia zaidi ushindi wa CCM
Wananchi walimpongeza kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa bwana Hassan Mtenga kwa kazi yake nzuri kuelekea kulitwaa jimbo la Iringa mjini,pamoja na aliekua mgombea wa chama hicho kata ya Nduli.
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa Chadema ambae alikuwepo eneo la Nduli akifuatilia matokeo ya uchaguzi huo pamoja na wafuasi wa Chadema alilazimika kuondoka katika eneo hilo baada ya kubaini kuwa hali ya ushindi kwa Chadema si shwari.
Wakati huo huo katika kata ya Njombe mjini mgombea wa Chadema amempiku mgombea wa chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo matokeo yanaonyesha mgombea wa CCM amepata kuongoza kituo kimoja pekee kwa tofauti ya kura 2 huku vituo vyote Chadema ikiibuka kidedea.
No comments:
Post a Comment