WAZIRI AMSHUSHA CHEO AFISA ELIMU SHULE ZA SEKONDARI MBINGA-RUVUMA
Naibu waziri wa elimu Kassim Majaliwa akiongea na walimu
NAIBU Waziri wa
Elimu na
Mafunzo ya Ufundi,ofisi ya Waziri mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Kassim Majaliwa amemvua madaraka kwa kumshusha cheo afisa elimu shule za sekondari wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Hanji
Yusuph Godigodi kwenda kuwa mwalimu wa kawaida wa sekondari kutokana na afisa huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kazi na
kufanya ubadhirifu wa shilingi milioni 268 za maendeleo ya elimu ya
sekondari wilayani humo.
Aidha amewashusha vyeo Wakuu wa shule za sekondari sita za wilaya hiyo kwenda kuwa walimu wa kawaida, kutokana na walimu hao wakidaiwa
kushirikiana na Ofisa huyo wa sekondari kufanya ubadhirifu wa fedha hizo.
Hatua ya Naibu Waziri huyo kuwashusha vyeo viongozi hao ilifikiwa katika kikao ambacho alikuwa akizungumza na Walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani humo, ambacho kiliketi kwenye ukumbi wa Uvikambi uliopo mjini hapa na kwamba Waziri huyo yupo katika ziara yake ya kikazi wilayani Mbinga kwa muda wa siku mbili.
Waziri Majaliwa aliwataja wakuu wa shule za sekondari wilayani Mbinga ambao wameshushwa madaraka kuwa ni William Hyera ambaye ni wa shule ya
sekondari Maguu, Clemence Sangana anatoka shule ya sekondari Mkuwani, Method Komba Langilo sekondari, John Tillia Ukilo sekondari, Leonard Juma Luli Sekondari huku akimtaja kwa jina moja mwalimu Konga ambaye yupo sekondari ya Kihangimahuka.

No comments:
Post a Comment