FAIDA ZA PAPAI MWILINI
HUIMARISHA MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai limeonesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya
ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo
katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa
usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na
madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari
ya kupatwa na kansa ya tumbo.
KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu
wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na
kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho
muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu
wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu
haraka na kupona.
KINGA YA MWILI
Vitamin
C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina
ya ‘beta-carotene’ kilichomo kwenye papai, ni muhuimu sana kwa
kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara
kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohoo, n.k
NURU YA MACHO
Kama
karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni
miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili
hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo
hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.
TIBA YA MAPAFU
Kama
wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako
unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye
kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na
madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
HUTUKINGA NA SARATANI YA KIBOFU
Ulaji
wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya
kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi
karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition
umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili
tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.
No comments:
Post a Comment