Sunday, 9 February 2014

LA LIGA: Real Madrid yaifunga Villarreal 4-2


Timu ya REAL Madrid imeifumua mabao 4-2 Villarreal katika mchezo wa La Liga usiku wa jana na kupanda kileleni mwa ligi hiyo. Cristiano Ronaldo hakushiriki mchezo hou kutokana na kuanza kutumikia adhabu yake ya mechi tatu.


Gareth Bale Real Madrid Goal Celebration

Gareth Bale

Mabao ya Real jana yamefungwa na mchezaji ghali duniani Gareth Bale dakika ya saba, Karim Benzema aliipatia timu yake bao jingine dakika ya 25 na 76 na Jese katika datika ya 64.

Kwa ushindi huu unaifanya Real itimize pointi 57 sawa na Atletico Madrid baada ya kila timu kucheza mechi 23, Real Madrid inapanda kileleni kutokana na wastani wake mzuri wa mabao.

Barcelona yenye pointi 54 baada ya kucheza mechi 22, inaweza kurejea kileleni ikiifunga Sevilla leo kwa kuwa inawazidi wastani mzuri wa mabao Real na Atletico.

http://agent108.biz/wp-content/uploads/2014/02/Prediksi-Real-Madrid-vs-Villarreal-9-Februari-2014-Liga-Spanyol.jpg

No comments:

Post a Comment