Sunday, 16 February 2014

MAANDAMANO NCHINI VENEZUELA

Watu wawili wauwa huku wengine 23 wakijeruhiwa katika maandamano nchini Venezuela mzozo wa kiuchumi uliogeka ghasia ukitajwa kua ndio chanzo.

Polisi nchini humo wamekabiliana na waandamanaji wa upinzani katika barabara za mji mkuu wa Carcas ambao wanataka kuachiliwa huru kwa wanafunzi waliokamatwa wiki iliopita.

Polisi wa kukabiliana na ghasia walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya huku waandamanaji hao wakiwatupia mawe.
Awali maelfu ya wafuasi wa Rais Nicholas Maduro pia walishiriki katika maandamano ya kuwapinga waandamanaji hao katikati mwa mji mkuu wa Carcas.

Raisi Maduro ameushtumu upinzani kwa kuzua fujo kwa lengo la kutaka kuipindua serikali yake.
Watu watatu waliuawa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali siku ya jumatano.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry ,ametoa taarifa akiitaka serikali ya bwana Maduro kuwaachilia huru wafungwa wote waliokuwa wakiandamana mbali na kuheshimu uhuru wa kujieleza.

No comments:

Post a Comment