Saturday 22 February 2014

FAIDA ZA ALOEVERA

 FAIDA ZA ALOE VERA AU SHUBIRI MWILINI

 
Licha ya ladha yake chungu, mmea wa aloe vera ukilimwa kwenye rutuba sahihi, kutunzwa vizuri na kusindikwa kwa uangalifu huwa na faida nyingi kwani una vichocheo chekwa vinavyoua vimelea vya magonjwa kama bakteria, virusi na fangasi.


Mtandao wa Mediclinic unaeleza kuwa Aloevera, huchochea utengenezwaji wa chembechembe mpya na tishu mpya zenye afya. Hufanya mfumo wa fahamu kufanya kazi vizuri na kutuliza matatizo yanayoathiri mfumo wa fahamu. Huondoa sumu mwilini na kufanya utendaji kazi wa mwili urudi katika hali ya kawaida.


Pia, husaidia kujenga seli mpya baada ya majeraha ya moto, kujikata, michubuko, vidonda vya tumbo, kung’atwa na wadudu wakali na wanyama. Husaidia matatizo ya kutopata haja, pia maumivu wakati wa haja kubwa na ndogo. Huondoa matatizo ya ngozi kama pumu ya ngozi (eczema), chunusi (acne) na fangasi.


Ni msaada kwenye umeng’enyaji wa chakula, kuongeza kinga ya mwili, kuondoa maumivu sehemu mbalimbali za mwili, matatizo ya usingizi, uchovu wa mwili usioeleweka, ugonjwa wa koo na pumu.

Hutibu matatizo ya kuhara na kutopata haja kubwa kiurahisi, hutibu sukari, vidonda vya tumbo.


Wanaume wengi wanaosumbuliwa na matatizo ya kuziba kibofu cha mkojo na pia kinamama wanao sumbuliwa na uambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI) ambayo huwafanya misuli ya kuzuia mkojo kulegea, mapafu, kusafisha maini na kuondoa sumu kwenye ngozi, aloe vera ni tiba.


Ili kupunguza uchungu, unaweza kutengeneza juisi yake na kuichanganya na asali ya nyuki wadogo.

No comments:

Post a Comment