Thursday, 13 February 2014

 FAIDA ZA TANGAWIZI MWILINI



 

 Tangawizi

Tangawizi ina umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu. Sana sana tangawizi hutumika kama kiungo katika mapishi. Manufaa yake kiafya ni kama ifuatavyo.
Tumbo: Tangawizi inatumika kutuliza maumivu ya tumbo, yanayotokana na matatizo ya usagaji chakula, kuharisha, kuvimbiwa, n.k. Inapotumiwa katika chakula tangawizi husaidia usagaji chakula. Aidha tangawizi humuongezea mtu hamu ya kula.

Kichefuchefu na Kutapika:
 Utafiti unaonyesha kuwa tangawizi ni tiba mufti kwa matatizo haya. Aidha huweza kutumiwa kupunguza tapishi inayotokana na uja uzito.

Matatizo ya Moyo:
 Tangawizi huimarisha moyo wa binadamu na kumwepushia maradhi ya moyo. Hii ni kwa kuwa inapunguza kiwango cha mafuta mwilini.

Matatizo ya Kupumua:
 Huondoa homa ya mafua, hutumika kutibu pumu, na pia kufungua mfumo wa upumuaji hasa inapotumika pamoja na asali.

Maumivu:
 Huondoa maumivu ya misuli, kichwa, na shinikizo la mawazo, kisunzi, na kukosa umakini.

Maumivu ya Hedhi:
 Hupunguza maumivu ya wakati wa hedhi.

Malaria:
Husaidi kutibu Malaria na Homa ya Manjano.

Nguvu za Kiume:
Tangawizi husaidia kuongeza nguvu za kiume kwa kutibu tatizo la mwanamume kutoa shahawa haraka.

Figo:
Inaaminika kuwa tangawizi inatibu tatizo la vijiwe vya kwenye figo.

Nywele:
Aidha hutumiwa kutunza nywele, kwa kuwa huondoa uyabisi (Dandruff.)

No comments:

Post a Comment