Saturday, 15 February 2014

SOMALIA: ALISHAAB WAPATA SILAHA ZA SERIKALI



http://thecontinentobserver.com/wp-content/uploads/2013/09/052813_AlShabab_16x91.jpg


Kutoka Somalia ripoti ya umoja wa mataifa imeonya kuwa silaha zilizokuwa zikipelekwa kwa vikosi vya serikali ya Somali zimeingia katika mikono ya kundi la Alshabaab kutokana na ukiukwaji wa utaratibu katika serikali.

Uchunguzi huo uliofanywa na wataalam walio huru umesema kuwa silaha za kudungua ndege,mabomu na risasi zilizotoka nchini Uganda na Djibout haziwezi kuwajibikiwa.
Ripoti hiyo sasa inataka taifa la Somali kuwekewa vikwazo vya silaha ambavyo viliondolewa mwaka uliopita.

Wataalam hao wamesema kuwa wana ushahidi kwamba mshauri mkuu wa rais nchini Somali amekuwa akihusika na mpango wa kuwapelekea silaha wapiganaji wa Alshabaab.

No comments:

Post a Comment