Monday, 10 March 2014

UN KUCHUNGUZA GHASIA CAR

UN KUCHUNGUZA GHASIA CAR

 

Umoja wa Mataifa umeanzisha uchunguzi wa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu kutokana na ghasia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati .

Mkuu wa kikosi cha uchunguzi Bernard Acho Muna, alisema kuwa kuwepo kwa wachunguzi nchini humo kutasaidia kuzuia mauaji ya kimbari.


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, liliamuru uchunguzi huo mwezi Disemba kuweza kutambua washukiwa ambao watafunguliwa mashitaka kuhusiana na ghasia hizo.

Maelfu ya watu wameuawa katika mzozo huo kati ya wapiganaji waisilamu na wakristo.



Shirika la chakula duniani linasema kuwa takriban watu milioni 1.3 ambao ni robo ya wananchi wa taifa hilo wanahitaji msaada.

"lazima tukomeshe tabia ya watu kufanya mambo bila kujali, '' alisema Bernard Acho Muna,jaji wa Cameroon,anayeongoza uchunguzi huo.



Alisema kuwa propaganda ya chuki nchini CAR, ni sawa na kilichofanyika nchini Rwanda kabla ya mauaji ya Kimbari mwaka 1994 ambapo takriban watu 800,000.

"hatutasubiri hadi mauaji yatakapofanyika ndipo tuchukue hatua ,'' alisema bwana Muna.



Maelfu ya waisilamu wametoroka huku wapiganaji wa kikristo wakifanya mashambulizi zaidi dhidi yao tangu kung'atuka kwa Rais wa kwanza muisilamu Michel Djotodia,mnamo mwezi Januari.



Rais wa mpito, Catherine Samba-Panza, mkristo, amesihi pande hizo mbili kukomesha ghasia, ingawa bado hali ni mbaya.



Wapiganaji wakristo wanasema kuwa wanalipiza kisasi kwa mashambulizi waliotendewa na wapiganaji waisilamu baada ya Djotodia kuchukua mamlaka mwezi Machi mwaka .
2013.
Waisilamu wengi wamevuka mpaka na kuingia katika nchi jirani za Cameroon na Chad, wakati mael;fu wangali wanaishi katika kambi za wakimbizi.

No comments:

Post a Comment