HALI KATIKA MITAA YA TRIPOLI SI SHWARI
Ripoti kutoka mji mkuu wa Libya, Tripoli, zinaeleza
kuwa mapambano mengine yametokea siku moja baada ya watu wengi kuuwawa
na kujeruhiwa kwenye maandamano ya kupinga makundi ya wanamgambo.
Ghasia zinatokea katika mitaa ya mashariki mwa Tripoli baina ya wanamgambo wa mji na wapiganaji kutoka mji wa Misrata.
Katika ghasia za Ijumaa wanamgambo wa Misrata
walifyatua risasi dhidi ya waandamanaji waliodai kuwa wanamgambo hao
waondoke Tripoli.
Wizara ya Afya inasema watu 43 waliuwawa Ijumaa
na 500 kujeruhiwa kwenye ghasia hizo, ambapo waandamanaji nao walijibiza
shambulio dhidi ya wanamgambo.
Waziri Mkuu, Ali Zeidan, ameziomba pande zote mbili kuwa na ustahmilivu.
No comments:
Post a Comment