WAZIRI MKUU LIBYA AZUIWA KUSAFIRI
Kiongozi wa mashtaka Nchini Libya Abdel-al-Qader
Radwan amemzuia Waziri mkuu wa taifa hilo aliyevuliwa madaraka, Ali
Zeidan, kusafiri nje ya taifa hilo hadi pale uchunguzi dhidi yake
utakapokamilika.
Anatuhumiwa kwa madai ya ubathirifu wa pesa za umma.
Bwana
Zeidan amesimamishwa kazi mapema siku ya Jumanne na Bunge la taifa
hilo, baada ya Wabunge kudai kuwa meli ya mzigo ya Korea Kaskazini
iliyokuwa imezuiliwa baada ya kunaswa ikibeba mafuta ghafi toka bandari
moja linalokaliwa na waasi huko Libya, ilivunja nanga na kusafiri
baharini.
Kura ya kutokuwa na imani na Bwana Zeidan
iliitishwa baada ya meli hiyo iliyokuwa na bendera ya Korea Kaskazini
kuabiri na kufikia maji makuu ya mipaka ya kimataifa baharini.
Mafuta hayo yalikuwa yamenunuliwa kutoka kwa waasi wanaodhibiti bandari ya Al- Sidra.
Wabunge hawana imani na Waziri Mkuu
Bunge la Libya limemuachisha kazi Waziri huyo mkuu, baada ya kupitisha agizo la kutokuwa na imani naye.
Hilo limeafikiwa baada ya meli ya Korea
Kaskazini kuingia katika bandari ya taifa hilo na kuondoka na mafuta
ghafi bila idhini ya serikali.
Makundi ya wapiganaji yamekuwa yakidhibiti
baadhi ya bandari ya taifa hilo mashariki mwa taifa, tangu Julai mwaka
jana na kuuza mafuta nje ya taifa.
No comments:
Post a Comment