MABAKI YA NDEGE ILIYOPOTEA YAONEKANA
Serikali ya Uchina imechapisha picha zilizonaswa na
mtambo wake wa satelite zikionyesha mabaki ya kitu kipana kikielea
katika bahari ya Kusini mwa Uchina.
Picha hizo zilipigwa siku ya Jumapili, saa
ishirini na nne baada ya ndege ya abiria ya Malaysia kutoweka ikiwa na
abiria 239, lakini haijabainika ikiwa vifaa hivyo ni vya ndege hiyo.
Huku
ikiwa na raia wake 154, ambao walikuwa abiria kwenye ndege hiyo ya
Malaysia, serikali ya Uchina imetuma mitambo kumi ya satellite kusaidia
katika harakati za kutafuta ndege hiyo.
Picha za vifaa hivyo vitatu, ambavyo moja ina
upana wa takriban mita 24 kwa 22, zilichukuliwa siku ya Jumapili, siku
moja tu baada ya ndege hiyo kupotea, lakini zilichapishwa siku ya
Jumatano.
Picha hizo za satellite zimeweka vifaa hivyo
takriban maili mia moja kutoka kwa njia iliyotarajiwa kutumiwa na ndege
hiyo na sio mbali kutoka kwa kisima kimoja cha mafuta, ambako mfanyakazi
mmoja aliripoti kuona kitu kilichokuwa kikichomeka angani siku ya
Jumamosi asubuhi.
Lakini siku chache zilizopita, kumekuwa na fununu kadhaa kuhusiana hatma ya ndege hiyo lakini zote zimekuwa uongo.
Makundi ya uokozi hiyo vile vile wanatafuta
mabaki ya ndege hiyo katika maji inayokaribiana na rasi ya Malaysia, kwa
sababu wanaamini kuwa ndege hiyo ya Malaysia ilibadili mkondo na
kuelekea Magharibi.
No comments:
Post a Comment