MAFURIKO YALETA MAAFA NIGERIA
Zaidi ya watu 50 wamefariki nchini Burundi baada ya kusombwa na maji pamoja na maporomoko ya udongo.Kwa mujibu wa waziri wa usalama, mvua kubwa ilinyesha usiku kucha katika mji mkuu Bujumbura na kusababisha uharibifu mkubwa.Majumba yamebomoka kufuatia mvua hiyo kubwa.
Waziri Gabriel Nizigama amesema kuwa tayari
wamepata miili ya watu 50, waliofariki baada ya nyumba zao kuporomoka na
kusombwa na maji.
Mitaa na vitongoji vya mji mkuu Bujumbura viliopo kaskazini vimeathirika zaidi.
Serikali ya Burundi mbali na kutangaza kwamba
itagharamia mazishi na huduma kwa majeruhi, imetangaza pia siku moja ya
maombolezi ya kitaifa siku ya Jumanne.
Baadhi ya walioshuhudia shughuli za uokozi
Miongoni mwa tarafa ambazo zimeathirika sana ni
Kamenge sehemu inayopakana na mkoa wa Bujumbura.
Inaarifiwa watu wengi
hususan watoto wamepoteza maisha.
Majeruhi wamelazwa katika hospitali kuu za serikali mjini Bujumbura na hasa Hospital Roi Khaled.
Na kutokana na uhaba wa nafasi katika vyumba vya
kuhifadhi maiti, baadhi ya maiti zimezikwa leo,kwa idhini ya familiya
zao na shughuli za uokozi zinaendelea lakini zinakabiliwa na ukosefu wa
vifaa, inasadikiwa kuwa maiti nyingi bado zimenaswa katika vifusi vya
majumba.
No comments:
Post a Comment