VIFUSI VYA NDEGE VYAONEKANA AUSTRALIA
John Young meneja mkuu wa halmasshauri ya usalama wa ndege nchini Australia
Waziri mkuu wa Australia amesema kuwa mitambo ya
satelite ya nchi hiyo imenasa picha za vitu vinavyoonekana kama vifusi
ambavyo huenda ni vya ndege ya Malaysia iliyopotea siku 13 zilizopita.
Waziri mkuu huyo, Tony Abbott, ameambia bunge
mjini Canberra kwamba picha za Satelite zimeonyesha vitu viwili
vinavyofanana na vifusi vya ndege hiyo. Taarifa hii imejitokeza karibu wiki
mbili baada ya ndege hiyo kutoweka na abiria zaidi ya miambili kutoka
mjini Kuala Lumpur Malaysia kuelekea Beijing.
Msemaji wa halmashauri ya usalama wa safari za
ndege, John Young, baadaye alisema kuwa vifaa hivyo ambavyo kimoja kina
ukubwa wa mita 24, vimeonekana umbali wa kilomita 2500 kusini Magharibi
mwa pwani ya Australia.Aliongeza kwamba,vifusi itakuwa vigumu kuviona vifusi hivyo na pia huenda sio vya ndege hiyo.
Wakati taarifa hii ilipotolewa, kulikuwa na
ndege ya Australia katika neo hilo , ndege zaidi zinatarajiwa kuwasili
katika eneo lenyewe na pia manowari ya jeshi inaelekea huko.
No comments:
Post a Comment