OBAMA ATOA ONYON KALI KWA URUSSI
Rais wa Marekani Barrack Obama, ameonya Urussi
kusitisha mpango wake wa kutaka kutwaa eneo la Crimea nchini Ukraine
lasivyo iwekewe vikwazo.
Akiongea katika Ikulu ya White House baada ya
kufanya mashauriano na kaimu Waziri Mkuu wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk,
rais Obama amesema nchi moja haiwezi kulazimisha taifa lingine kwa mtutu
wa bunduki.
Bwana Yatsenyuk amesema taifa lake sasa ni sehemu ya mataifa ya Magharibi na kamwe haliwezi kurudi nyuma.
Mabalozi katika Umoja wa Mataifa, wanasema
Mataifa ya Magharibi yanaandaa azimio la pamoja, katika baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo litakariri uhuru wa taifa la Ukraine
na pia kuangazia kuhusu kura ya maoni kuhusu itakayofanyika siku ya
Jumapili, ikiwa eneo hilo la Crimea litajitenga na kuwa sehemu ya
Urussi.
Hata hivyo inatarajiwa kuwa Utawala wa Moscow
utatumia kura yake ya turufu katika baraza hilo la Umoja wa Mataifa
kupinga azimio hilo.
No comments:
Post a Comment