MKUU WA JESHI KUGOMBEA URAISI MISRI
Mkuu wa majeshi na waziri wa ulinzi Misri, Abdul
Fattah al-Sisi, ametangaza kujiuzulu jeshini ili kugombea katika
uchaguzi wa urais mwezi ujao.
Wagombea wote wanapaswa kuwa raia.
Akizungumza Kwenye hotuba ya
Televisheni huku akiwa amevalia sare ya kijeshi Abdel Fattah El Sissi
amesema yeye sio mwanajeshi tena baada ya miaka 44 na kwamba amechukua
hatua hiyo ili aweze kutimiza jukumu lingine muhimu.
Ni Bayana kwana Sisi hatakua na kibarua kigumu
kujipatia ushindi katika uchaguzi wa Urais. Anaungwa mkono na idadi
kubwa ya raia wa Misri na hadi sasa hana wapinzani wowote.
Baadhi ya waliotaka kugombea urais wamejiondoa wakidai kwamba hawataweza kuendesha kampeni zao kwa njia huru.
Wafuasi wake Sisi wanamuona kama kiongozi imara
ambaye anaweza kurejesha amani na udhabiti nchini Misri baada ya miaka
mingi ya machafuko.
Wakosoaji wake wanasema ana msimamo mkali na amechangia pakubwa katika kusambaratisha na kuhujumu upinzani nchini Misri.
Mkuu huyo wa jeshi atakabiliwa na majukumu
mazito ya kufufua uchumi uliofifia , kupambana na uasi na kuileta pamoja
nchi iliyogawanyika. Ameahidi kutekeleza mabadiliko makubwa lakini
akaonya kuwa hawezi kufanya miujiza.
No comments:
Post a Comment