NICOLAS ANELKA ATIMULIWA WEST BROM
Mchezaji wa klabu ya soka ya West Brom, Nicolas Anelka amefutwa kazi kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Klabu hiyo iliamua kuchukua hatua hiyo baada ya Anelka kutangaza kupitia mtandao wa kijamii kuwa anaacha kazi.
Anelka alisema kuwa anaondoka katika
klabu hiyo baada ya kukosa kutatua tofauti zilizopo kati yake na Albion
kuhusu ishara yake yenye utata ambayo inasemekana kuwa ya kibaguzi
dhidi ya wayahudi.
Mshambuluaji huyo mwenye umri wa miaka 35,
alipigwa marufuku kutocheza mechi tano na kutozwa faini ya pauni 80,000
na shirikisho la soka Uingereza ,kwa kufanya ishara hiyo, baada ya
kuingiza bao dhidi ya klabu ya West Ham mwezi Disemba.
West Brom imechukua hatua ya kumfuta kazi Anelka
kutokana na ishara hiyo na pia kwa sababu ya matamshi yake kwenye
mtandao wa kijamii.
Ishara hii inapigiwa debe na msanii wa Ufaransa Diedonne M'bala M'bala
Awali aliachishwa kazi mwa muda na Albion, wakati klabu hiyo ilipokuwa inafanya uchunguzi wake binafsi.
Mapema siku ya Ijumaa, Anelka alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa anaondoka katika klabu hiyo.
Aliandika: "kufuatia mazungumzo kati yangu na
maafisa wa klabu, kuna masharti kadhaa ambayo wamenipa kabla ya kujiunga
tena na klabu hiyo, Masharti ambayo siwezi kuyakubali.''
Hata hivyo klabu ilisema kuwa masharti
yaliyotolewa kwa Anelka ni pamoja na kumtaka awaombe msahama mashabiki ,
wadhamini na jamii kwa ujumla kwa athari iliyotokana na ishara yake
aliyoifanya Disemba tarehe 28 na pili akubali kutozwa faini.
No comments:
Post a Comment