MAGEUZI CHINA NI LAZIMA
Waziri mkuu wa China, Li Keqiang, ameuambia mkutano
wa kila mwaka, wa bunge la taifa hilo mjini Beijing, kwamba maendeleo ya
kiuchumi yatabaki kuwa jukumu kubwa zaidi la serikali, lakini
marekebisho ya kimsingi ni sharti yatekelezwe japo ni machungu.
Bwana Li amewaambia maelfu ya wajumbe katika
bunge la taifa hilo, Great Hall of the People, kwamba shabaha ya kila
mwaka ya ukuaji wa kiuchumi itasalia kuwa asilimia saba nukta tano.
Akizungumzia tatizo la uchafuzi, amesema kuwa
moshi mkubwa unaondelea kutanda katika miji mikubwa ya China, ni onyo la
kiasili dhidi ya maendeleo yasiokuwa na mpango.
Waziri huyo mkuu wa China kadhalika ametangaza
marufuku dhidi ya majengo mapya ya serikali kama sehemu ya kile
alichokitaja kuwa mapambano bila huruma dhidi ya ufisadi.
No comments:
Post a Comment