RAISI OBAMA KUKUTANA NA PAPA ROMA
Rais Barrack Obama wa Marekani anatarajiwa kukutana
na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, katika makao yake
makuu huko Vatican.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Obama kukutana na papa Francis.
Wawili hao wanatarajiwa kujadili namna ya
kupunguza tofauti iliyopo kati yao katika maswala mengi mbali na
kujaribu kuinua maisha ya watu maskini duniani baada ya takwimu
kuonyesha kuwa tofauti ya mapato kati ya matajiri na Masiki inaendelea
kupanuka .
Aidha viongozi hao wawili wanatazamiwa kujadili hali ilivyo Nchini Ukraine, na swala la upatikanaji wa amani mashariki ya kati.
Mwafaka baina ya mitazamo tata kuhusiana na
maswala ya uavyaji mimba, matumizi ya dawa za kupanga uzazi na ndoa ya
jinsia moja pia inatarajiwa kuwa kati ya mada itakayojadiliwa .
No comments:
Post a Comment