Wednesday, 12 March 2014

MH370 ILIBADILI MKONDO


 

Mkuu wa jeshi la anga la Malaysia, amekanusha madai kuwa ndege ya Malaysia iliyotoweka, ilionekana mara ya mwisho Magharibi ya rasi ya nchi hiyo, eneo ambalo ni mbali zaidi na njia iliyostahili kupita.


Generali Rodzali Daud, amesema kuwa hawawezi kupuuza uwezekano huo, lakini amesema madai kuwa mawasiliano ya ndege hiyo yalinaswa na mtambo wa radar katika eneo hilo sio kweli.


Amesema mawasiliano ya mwisho ya ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing yalinaswa katika rasi iliyoko kati ya Malaysia na Vietnam.


Ndege na meli kadhaa zimekuwa zikitafuta mabaki ya ndege hiyo katika eneo la bahari ya Malaysia, lakini hazijafanikiwa kupata mabaki ya ndege hiyo.

Msako unaendelea

Jeshi la Malaysia limesema kuwa, mtambo wake wa radar unaashiria ndege hiyo iliyotoweka, ilielekea eneo la Magharibi, mbali na njia iliyostahili kupita kabla ya kutoweka.


Ndege hiyo MH370 ilitoweka siku ya Jumamosi, baada ya kupaa ikiwa na abiria mia mbili na thelathini tisa.
Juhudi za kimataifa za kutafuta ndege hiyo zimepanuliwa na kuimarishwa.


Awali ilibainika kuwa watu wawili waliokuwa wakisafiri kwa kutumia paspoti zilizoibiwa walikuwa raia wa Iran ambao hawana uhusiano na kundi lolote la Kigaidi.

No comments:

Post a Comment