LIVERPOOL YAICHAPA MANCHESTER UNITED
Katika kile kilichoonekana kama harakati za kushinda taji lao la
kwanza tangia mwaka 1990,Liverpool ilipita mtihani wao kwa kuonyesha
mchezo mzuri dhidi ya timu ya Manchester United ambayo haikuweza
kuwadhibiti wapinzani wao na hivyobasi kusogea hadi nafasi ya pili na
pointi nne nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Chelsea.
Nahodha wa Liverpool Gerard alionyesha uongozi wake huku wakifazawadiwa mikwaju ya penalty katika vipindi vyote viwili huku timu hiyo ya meneja Brenda Rodgers ikitawala dhidi ya timu ya Machester ambayo inahitaji marekebisho makubwa.
Kutokana na mechi hizo za leo Chelsea iko katika
nafasi nzuri ya kushinda taji hilo kwa alama 66 ikiwa imecheza mechi 30
huku timu za liverpool na Arsenal zikiwa na pointi 62 kila mmoja,
lakini liverpool inashikilia nafasi ya pili kwa wingi wa mabao.
Arsenal ni ya tatu huku Manchester City iliocheza mechi 27 ikiwa na pointi 60 na hivyobasi ikifunga udhia wa time nne bora.
No comments:
Post a Comment