HALI BADO SI SHWARI BUNGE LA KATIBA
Bunge Maalum la Katiba lipo njiapanda baada ya kuwapo mivutano isiyoisha
miongoni mwa wajumbe huku kukiwa na taarifa kwamba ikiwa leo muafaka
kuhusu upigaji kura hautapatikana, baadhi ya wajumbe watajiuzulu.
Ikiwa hali hiyo itatokea, uwezekano wa Mkutano wa Bunge hilo kuendelea ni mdogo hivyo linaweza kuvunjika.
Taarifa za uhakika kutoka Dodoma zinaeleza kuwa baadhi ya wajumbe
wanataka kura ya leo inayolenga kuamua juu ya kanuni za bunge hilo
katika kupitisha rasimu ya katiba iwe ya siri au ya wazi, nayo iwe ya
wazi.
“Kwa kweli hadi sasa tuna zaidi ya majina 250 ya wajumbe ambao wanapinga
vikali jaribio lolote la kutaka kura ya kumua kanuni leo iwe ya wazi
badala ya siri. Hili likitokea nafikiri Bunge hili litakuwa limefikia
ukomo,” kilisema chanzo chetu kutoka Dodoma na kuongeza kuwa:
“Yaani ni mambo ya kushangaza saba, Chama Cha Mapinduzi inaelekea
kimetoa maelekezo kuhusu hali hii. Waameamu kutumia njia hii kuwatisha
wabunge. Wanataka kutumia wingi wao vibaya kushawishi vitu ambavyo
havina maana.”
Kutokana na mvutano huo, wajumbe hao wameazimia kuwa leo watajiuzulu
ujumbe kwenye Bunge hilo kwa madai kwamba wenzao hasa wanaotoka CCM,
wanataka kura ya wazi kuamua mgogoro uliokuwa umetokea wiki iliyopita
kuhusu upigaji kura wa kupitisha rasimu ya kanuni zitakazosimamia
uendeshaji wa Bunge hilo.
No comments:
Post a Comment