POLISI WAUA DEREVA WA BAJAJI KWA KIPIGO
Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni limeingia katika kashfa baada ya
askari wake wa Kituo cha Stendi Kikuu ya Mabasi Ubungo (UBT), kutuhumiwa
kumpiga, kumjeruhi na kusababisha kifo cha dereva wa bajaji, Salehe
Said (19), maarufu kama ‘Kibange Moto’, mkazi wa Kigogo, jijini Dar es
Salaam.
Dereva huyo alikutwa na mkasa huo, Machi 24, mwaka huu, saa 7:00 usiku, huku kukiwa na utata wa eneo alilokutwa na mauti.
Utata huo unafuatia polisi kudai kuwa dereva huyo alifariki wakati akiendelea na matibabu, huku kikundi cha madereva wa bajaji cha Jitume cha Ubungo kikidai kuwa alifia mikononi mwa polisi.
Baadhi ya madereva wa bajaj walidai chanzo cha tukio hilo ni ugomvi kati ya marehemu na dereva teksi bubu uliotokana na kugombea abiria aliyefika katika eneo hilo kutafuta usafiri nje ya UBT.
Walidai kutokana na vuta nikuvute hiyo, wote wawili walikamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi.
Kwa mujibu wa madereva hao, Saleh aligoma kuingia mahabusu ya kituo hicho akitaka kwanza aambiwe kosa lake.
Walidai jambo hilo lilisababisha askari huyo (jina linahifadhiwa) kuanza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili na kuwa baada ya kipigo hicho, baadhi ya madereva wenzake walianza kumtetea, lakini nao walikamatwa na kuwekwa ndani.
Walidai baada ya muda mfupi, mwenzao aliyepigwa alianza kuvimba na polisi aliyempiga aliamua kumpeleka katika Hospitali ya Sinza Palestina, lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya.
“Wakati askari huyo amempiga dereva mwenzetu, walikamatwa wengine watano wakawekwa ndani, lakini hali ya mwenzetu ilipokuwa mbaya, askari walimchukua na kumpeleka katika Hospitali ya Palestina Sinza, lakini walipomrudisha kituoni, alizidiwa. Wakamrudisha tena hospitali usiku huo huo,” alisema mmoja wa madereva hao.
Aliongeza: “Mara ya kwanza walivyompeleka hospitali, walitumia bajaj ya mwenzetu, ambaye naye alikuwa amewekwa ndani, lakini mara ya pili hali ilipozidi kuwa mbaya, walimrudisha hospitali na hawakumrudisha tena kituoni.”
Kijana huyo alisema Jumanne asubuhi baada ya kwenda kituo cha polisi cha UBT walikokuwa wameshikiliwa wenzao, waliambiwa kuwa walikuwa wamehamishiwa kituo cha Magomeni Usalama.
Alisema baada ya kwenda kituo cha Usalama, waliwakuta wenzao wanne, ambao waliwaeleza kwamba, mwenzao aliyekuwa amepigwa alipelekwa hospitali usiku na hakurudishwa tena kituoni.
Alisema walipowauliza polisi mwenzao aliko, hawakutoa jibu lolote na ndipo waliamua kufuatilia katika hospitali waliyokuwa wamempeleka, lakini hawakumuona na hivyo kuanza kumtafuta katika hospitali nyingine.
“Tulipokosa jibu la wapi alipo mwenzetu kutoka kwa askari, tuliamua kutembelea kila hospitali. Tulipofika Mwananyamala kwenye wodi, napo tulimkosa. Tukaamua kwenda mortuary (chumba cha kuhifadhi maiti). Tukakagua daftari na ndipo tukaona jina lake,” alisema.
Aliongeza: “Kwa kweli ilituuma sana. Tena kibaya zaidi, maelezo yalikuwa yameandikwa kuwa kifo chake kimesababishwa na kupigwa.

Tunaomba sheria ichukue mkondo wake huyo askari achukuliwe hatua
kali. Na pia tunataka wenzetu waliokamatwa bila hatia, waachiwe kwa
sababu polisi wamewabambikia kesi ya wizi wakati siyo kweli.Pia faili
lake limeandikwa kwamba alipigwa na wananchi wenye hasira kali,
tumechoka kuonewa.”
Juzi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema hana taarifa zozote juu ya tukio hilo.Hata hivyo, jana alipoulizwa tena alisema: “Kifo cha dereva huyo hakikusababishwa na askari.”
Wambura alisema dereva huyo alikamatwa na kufikishwa kituoni kwa tuhuma za kumvamia afisa wa Benki ya ABC na kumpora na kuwa baada ya kukamatwa, alijaribu kutoroka, lakini alikamatwa tena na polisi kwa kushirikiana na watu wengine na kurudishwa kituoni.
“Kwanza naomba unielewe kwamba kifo cha dereva huyo, ambaye pia inasemekana ni ‘deiwaka’ wa bodaboda hakikusababishwa na polisi.

Bali alitaka kuwatoroka polisi baada ya kukamatwa kutokana na kosa la
kumvamia afisa wa ABC katika lango la kutokea stendi ya mkoa (UBT) na
kikundi cha madereva wanaopaki katika eneo hilo. Na kati ya waliohusika
na tukio hilo, ni pamoja na huyo marehemu,” alisema Wambura.
Alisema afisa huyo aliegesha gari lake akisubiri mgeni wake, lakini kikundi hicho kilimzongazonga na kuanza kumshambulia kisha kumpora Sh. 40,000, simu mbili na kadi za benki na kumchania nguo zake.
Wambura alisema afisa huyo aliripoti kituo cha polisi na baadaye askari walikwenda kuwakamata madereva hao.
Alisema majira ya saa 4:30 usiku, marehemu alizidiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Palestina Sinza.
Kwa mujibu wa Wambura, marehemu alirudishwa kituoni, lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya, hivyo kulazimika kurudishwa tena hospitalini hapo na baadaye Hospitali ya Mwananyamala na kwamba, ilipofika saa 7:00 usiku alifariki.
Wambura alisema kutokana na madai mbalimbali, wanafanya uchunguzi kujua chanzo hasa cha kifo hicho.

No comments:
Post a Comment