MSUKOSUKO WA AMANI SUDANI YA KUSINI
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini
na waasi wanaoongozwa na aliyekuwa naibu wa rais wa nchi hiyo Riek
Machar yanatarajiwa kuanza tena leo mjini Addis Ababa Ethiopia. Mazungumzo hayo yaliahirishwa mapema mwezi huu baada ya mazungumzo ya hapo awali kukwama.
Aidha, pande zote mbili zimetuhumiwa kwa kukiuka mkataba wa kusitisha mapigano uliotiwa saini mwezi Januari. Mnamo siku ya Jumatano, mataifa ya magharbi
yanayohusika na mgogoro huu wa Sudan Kusini katika kuutafutia suluhu la
kudumu, walitishia kuwawekea vikwazo wahusika wakuu kwenye mgogoro huo
ikiwa hawatausuluhisha.
Mazungumzo ya kuzipatanisha pande hizo hayajapiga hatua kwa wiki mbili zilizopita huku wahusika wakilaumiana. Serikali na waasi wanalaumiana kwa kuyumbisha mazungumzo ya amani. Nao mkataba wa amani uliotiwa saini kusitisha vita pia haujafanikiwa katika kumaliza mgogoro huo.
Baadhi ya wanadiplomasia kutoka nchi za
magharibi, wamehoji ikiwa viongozi wamejitolea kikweli kutafuta muafaka
huku kila mhusika akimlaumu mwenzake kwa kizungumkuti kilichoko.
Mazungumzo hayo yanaanza tena baada ya wiki
mbili ya kusitishwa kwake, ingawa wajumbe wamesema haijulikani ikiwa
pande hizo mbili zitakuwepo. Maswala makuu yanayoyumbisha mazungumzo hayo, ni
matakwa ya waasi wa Sudan Kusni kwamba wafungwa wanne wa kisiasa ambao
bado wanazuiliwa, sharti waachiwe huru.
Wanne hao walilaumiwa kwa kupanga njama ya
mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir wakiongozwa na aliyekuwa
makamu wa Rais Riek Machar.
No comments:
Post a Comment