HOTUBA MAALUM YA UFUNGUZI WA BUNGE LA KATIBA
Siku tatu baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Mstaafu Joseph Warioba, kutikisa Bunge Maalum la Katiba kwa hoja nzito
juu ya rasimu ya katiba, kesho mji wa Dodoma utarindima tena kwa
kufunikwa na viongozi wakuu wote wa kitaifa waliopo madarakani na
waliostaafu.
Ugeni huo umealikwa bungeni kushuhudia hotuba ya ufunguzi wa bunge hilo
la kihistoria itakayotolewa na Rais Jakaya Kikwete kesho kama sehemu ya
utekelezaji wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2012.
Tukio hilo litahudhuriwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.Wengine walioalikwa ni wajane wa waasisi, Mama Maria Nyerere na Fatma Karume.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana, Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, Yahaya Khamis Hamad, alisema kuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, amewaalika wageni mbalimbali ili kushuhudia tukio hilo muhimu la kitaifa.
Khamis aliwataja wageni wengine walioalikwa kuwa ni pamoja na marais wastaafu kutoka pande zote za Muungano. Marais wastaafu waliopo ni Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Dk. Salmin Amour Juma na Amani Abeid Karume.
Wengine ni maspika wastaafu, Waziri Kiongozi mstaafu ambaye hakutajwa jina. Hata hivyo, mawaziri kiongozi wastaafu waliopo ni Shamsi Vuai Nahodha ambaye ni Mjumbe wa bunge hilo, Ramadhan Haji Faki na Maalim Seif. Spika Mstaafu ni Pius Msekwa.
Waalikwa wengine ni watendaji wakuu kutoka pande zote za Muungano, mabalozi wa nchi mbalimbali waliopo nchini, wawakilishi wa taasisi za kimataifa pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za ndani ya nchi.
Alizitaja taasisi hizo kuwa ni taasisi za kidini, wawakilishi wa tasnia ya habari, vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu, taasisi zisizo za kiserikali, vyama vya watu wenye ulemavu, taasisi ya elimu, vyama vya Wafanyakazi, vyama vya wafugaji, vyama vya wavuvi, vyama vya wakulima na wawakilishi toka sekta binafsi.
Akizungumzia mpangilio wa shughuli hiyo, Khamis alisema kuwa Bunge litaanza kikao chake majira ya saa 9:10 jioni na baadaye kikao kitaahirishwa saa 9:20 kwa ajili ya kumpokea Rais.Khamis aliwataka wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na waalikwa wote kuwahi kuingia ndani ya ukumbi kabla Rais hajawasili kwenye viwanja vya Bunge.
Alisema baada ya Rais kuwasili katika viwanja vya Bunge, atapokewa na Mwenyekiti wa Bunge, Makamu wake, Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.Alisema baada ya mapokezi, Rais ataelekea kwenye Jukwaa maalum kwa ajili ya kupokea salamu ya heshma na kukagua gwaride Maalum ambalo limeandaliwa na Jeshi la Polisi.
Khamisi alisema kuwa tukio la kukagua gwaride hilo litakapokamilika, viongozi wataingia bungeni kwa maandamano maalum kwa ajili ya kwenda kusikiliza hotuba ya Rais ya kuzindua Bunge hilo.
Alisema viongozi watakaoshiriki maandamano hayo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atafuatana na Mwenyekiti wa Bunge Maalum.
Alisema Rais atakapomaliza kuhutubia, Wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba watapata fursa ya kupiga picha ya pamoja na Rais.Rais Kikwete anatarajiwa kuhutubia Bunge saa 10:00 jioni kwa mujibu wa kanuni ya 75 (1) ya Bunge Maalum la Katiba.
Ingawa maudhui ya hotuba ya Rais Kikwete hayajajulikana, hotuba ya Jaji Warioba bungeni juzi, imekuwa ni jambo zito ambalo yamkini yatagusiwa kwa mapana yake.
Miongoni mwa mambo nyeti na yamekuwa na ubishani mkubwa ambayo yameibuliwa na Tume na kuwekwa kwenye Rasimu ya Katiba ni pamoja na muundo wa Muungano wa serikali mbili, wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakipinga kwa nguvu zote.
Mambo mengine ni kupunguzwa kwa kiwango kikubwa kwa madaraka ya rais; kujenga uwajibikaji kwa kuweka maadili ya viongozi ndani ya katiba; kuimarishwa kwa haki za raia na kuwandoa mawaziri kuwa wabunge.
Hofu iliyokuwa imetanda mjini Dodoma ambayo ilisababisha hata Jaji Warioba kushindwa kuwasilisha hotuba yake Jumatatu, ni suala linaloonekana kama kuviziana na kukosekana kuaminiana baina ya wabunge wanaotokana na CCM na wale wa upinzani wakishirikiana na wa kundi la kuteuliwa lenye wajumbe 201.

No comments:
Post a Comment