12 WAJIUNGA KUISAIDIA MALAYSIA KUITAFUTA NDEGE
Wiki moja tangu ndege ya Malaysia iliyokuwa imewabeba
abiria 239 kutoweka, juhudi za kimataifa kuisaka ndege hiyo bado
zinaendelea.
Mataifa kumi na mbili sasa yamejiunga pamoja
kuisaidia serikali ya Malaysia na msako huo, juhudi
zaidi zikipelekwa Magharibi mwa rasi ya Malaysia.
Marekani imesema kuwa inatuma manowari zake za
kivita, pamoja na ndege maalum ya uchunguzi katika maeneo ya Bengal,
Bahari ya Andaman na sehemu za Bahari hindi.
Mnamo Ijumaa taarifa ziliibuka kuwa ndege hiyo
ilituma mawasiliano katika kituo cha trafiki ya ndege kwa karibu saa
tano baada ya taarifa ya kupotea kwake kutolewa.
Taarifa zinasema kuwa mawasiliano hayo yanaweza
kusaidia katika kujua iliko ndege hiyo na ndio maana Marekani ikaamua
kutuma meli zake za kivita katika Bahari Hindi.
No comments:
Post a Comment