MILIPUKO YATOKEA NIGERIA
Mji wa Maiduguri uliopo kazkazini mwa Nigeria
umekumbwa na milipuko miwili, huku ripoti zikiarifu kwamba takriban watu
10 huenda wamepoteza maisha yao.
Mkaazi mmoja ameliambia shirika la habari la
Ufaransa kwamba mlipuko wa kwanza ulitokea katika eneo lililojaa watu
huku wa pili ukilipuka wakati majirani walipokuwa wakiwasaidia
waathiriwa.
Maafisa wa polisi wamesema kuwa watu wengi wamekwama chini ya vifusi.
Mji wa Maiduguri hutumiwa kama kambi ya wanajeshi wanaopigana na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Awali ripoti zimearifu kuwa kulikuwa na shambulizi la angani katika kijiji kimoja cha jimbo la Borno siku ya ijumaa.
Shahidi mmoja ameiambia BBC kwamba takriban raia 20 wamefariki.
Jeshi la Nigeria linadaiwa kuvilipua vijiji inavyoamini ni makao ya wanachama wa Boko Haram.
No comments:
Post a Comment