KIKWETE ASEMA TUWAACHE WABUNGE WAAMUE SERIKALI MBILI AU TATU
Rais Jakaya Kikwete amesema amemaliza kazi ya kulihutubia Bunge Maalum
la Katiba na sasa anawaachia wabunge wa bunge hilo kujadili na kuamua
muundo wa Muungano unaofaa kama serikali mbili au tatu kwenye
mapendekezo ya Rasimu ya Katiba Mpya.
Rais Kikwete alielezea msimamo huo juzi wakati akizungumza na wazee katika Ikulu ndogo ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara yake ya siku moja wilayani hapa, alitoa msimamo wake baada ya wazee hao kumweleza kwenye risala yao kuwa wao wanataka serikali mbili. Risala hiyo ilisomwa na Mwenyekiti wa Wazee wa Wilaya ya Muheza, Hamisi Mzee.
Rais Kikwete alisema kwa sasa amewaachia wabunge kuamua muundo wa Muungano unaotakiwa na baadaye wananchi wataamua kama wanataka serikali tatu ama mbili wakati wa kupitisha Katiba.
Alisema kama watapendekeza serikali tatu ruksa kwani ndiyo mapendekezo yao, hivyo hayawezi kupingika kwa namna yoyote.
Hata hivyo, Rais Kikwetee alisisitiza kuwa lakini waelewe kuwa serikali tatu zina changamoto zake
No comments:
Post a Comment