UN YAILAANI MISRI KUHUSU HUKUMU YA KIFO
Umoja wa Mataifa umelaani kitendo cha Misri
kuwahukumu kifo zaidi ya watu miatano ikisema kuwa ni ukiukwaji wa
sheria za kimataifa za haki za binadamu.
Umoja huo umesema kuwa idadi ya watu
waliohukumiwa Jumatatu, ndio idadi kubwa ya watu kuwahi kuhukumiwa kifo
kwa wakati mmoja katika miaka ya hivi karibuni.
Mawakili wa utetezi wamesusia kesi ya pili ya
watu wengine karibu miasaba wafuasi wa Morsi wanaokabiliwa na tuhuma
sawa na zile zilizowakabili watuhumiwa wa kwanza.
Wamlalamikia kile wanachosema ni mahakama kukosa kufuata utaratibu unaofaa.
Kesi ya wafuasi wengine 682 waliosalia ilianza
kusikilizwa mapema leo lakini ikaahirishwa baada ya muda mfupi huku
jaji akisema kuwa hukumu itatolewa mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment