NGOME YA AL-SHABAABU YADHIBITIWA SOMALIA
Vikosi vya serikali ya Ethiopia na Somalia
vimedhibiti mji ulio katikati ya Somalia uliokuwa mikononi mwa
wanamgambo wa al-Shabaab, maafisa wameeleza.
Takriban watu 12 waliuawa katika mapigano makali
katika mji wa Radboore lililokuwa likizozaniwa lililo mjini Bakol,
wakazi wa eneo hilo wameshuhudia.
Vikosi vya Ethiopia ni sehemu ya Wanajeshi 22,000 wa Umoja wa Afrika (AU) wanaopambana na wanamgambo nchini Somalia.
Imeelezwa kuwa kudhibitiwa kwa mji wa Radhoore
ni hatua muhimu kwa kuwa ilikua ngome kuu ya al-shabaab katika
kutekeleza mashambulizi mjini humo.
Huu ni mji wa kwanza ambao al-Shabaab walipoteza
tangu mwezi Septemba, mji wa Mahaday ulipodhibitiwa toka mikononi mwa
al-shabaab.
Hivi sasa vikosi vinaelezwa kuwa vinaelekea mji wa Hudur ambao pia unadhibitiwa na al-Shabaab.
Wanamgambo hao wenye uhusiano na al-Qaeda, wanadhibiti eneo kubwa la katikati mwa Somalia.
No comments:
Post a Comment